Mwanangu Alikuwa Ananiuliza Baba Nifanye Kosa Gani ili Nije Tuishi Wote Gerezani – Lema

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema ambaye amesota gerezani kwa zaidi ya miezi minne, amefunguka kwa mara ya kwanza kuwashukuru wale waliompigania huku akieleza stori ya kusisimua kuhusu mtoto wake.

Lema amedai anaenda kumuona mwanaye ambaye alitaka kufikia uwamuzi wa kutaka kufanya kosa ili na yeye aingie gerezani kukaa na baba yake.

“Leo nina mambo machache sana ya kuongea, ninamshukuru sana mwenyezi Mungu, mke wangu, familia yangu, mawakili, viongozi wa chama na wananchi wote waliokuwa na mimi. Na kwa namna ya pekee mke wangu, kama ningepata nafasi ya kuoa tena, ningemuoa yeye. Pia mtoto wangu alifikia hatua akasema anatamani kufanya kosa ili aje alale na mimi gerezani, na akauliza ni kosa gani afanye ili aletwe gerezani,” alisema Lema.

Mbunge huyo ameachiwa kwa dhamana yenye masharti ya wadhamini wawili wanaoaminika pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 1.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad