Ukweli Mchungu...Ugumu wa Magufuli Kumtumbua Makonda Uko Hapa..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kama Mtanzania niishie Dar es Salaam kuna mambo hupaswi yakupite. Wengi walikuwa wakitegemea mheshimiwa Rais kumtupilia mbali Makonda/Bashite ila haijawa kama mategemezi ya wengi kuwa hivyo.

Hii inatokana na sababu mbalimbali kama zifuatazo

i) Vita ya Dawa za Kulevya. Wengi tunajua vita hii ilivyo ngumu na hii ndo iliomfanya mpaka siri zake zikafichuka na raisi mwenyewe akaisapport hiyo vita na kutaka iendelee. Sasa leo hii akimtumbua kwa visa vilivyoibuka kutokana na madawa ya kulevya itakuwa ni usaliti na kutokuwa na maana.

ii) Kuna watu wanaopinga kila kitu afanyacho Rais, hapa nasemea Instagram pamoja sana sana pamoja na wanasiasa wanaopinga kila kitu kinachofanywa. Imagine mtu anapinga hadi kuletwa kwa ndege au flyover zinajengwa mtu anapinga   (watanzania hatuko serious)

Kuna hadi wengine wanataka ufisadi urudi ili maisha yapungue ugumu. Wengine wakawa wanasema ni mpango wa ikulu kumtuma afanye hivyo ili wamtoe wafunike skendo na udhaifu wa serikali.

Mtu kama huyu utafata atakachokushauri na ina maana ukifata umempa kiburi aonekane yeye ndo yeye na atakaloamua nchi nzima inafata, liwe baya au zuri. Na mwenendo kama huo ungefanya serikali iwe dhaifu kupita kiasi

So ndo maaana Magufuli akaita hiyo call
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mtasubiri sana Makonda kutumbuliwa wauza unga nyie

    ReplyDelete
  2. ukiwa huwa cha kuongea kaa kimya........

    ReplyDelete
  3. Mlikuwa wapi siku zote kumchunguza Makonda? Hii ni dhahiri kuwa hakuna uzalendo hapa isipokuwa ni wauza unga kutetea matumbo yao. Mtu mwenye akili akifatilia sakata hili atajua tu kuwa kuna maslahi binafsi juu ya wanaoomba Makonda atumbuliwe!

    Kama mlizijua habari za Makonda kwa kiwango hicho kwa nini hamkumsaidia Rais alipomteua kuwa mkuu wa wilaya? Nakumbuka Baraza la Mitihani limekuwa likiiomba jamii iwasaidie kupeleka taarifa za watu wanaosemekana kuwa na vyeti feki kwa nini hamkufanya hivyo mpaka mtajwe kuwa wauza unga?

    Hata ukuu wa mkoa mliona anafaa kuongoza umma wa mkoa wenye watu wengi ili hali hana sifa hizo ila miliona ni sawa mkanyamaza. Uzalendo uko wapi hapo?

    Wakati anawatumbua wale maafisa ardhi wa Kinondoni kwa kuchelewa kufika eneo lililokuwa na mgogoro wa ardhi kwa nini pale napo hamkuona kama hakutumia busara kuwaweka ndani bila kuchunguza sababu ya kuchelewa kwao? Au kumuachia mkuu wao wa kazi kuwawajibisha kulingana na taratibu na maadili ya kazi zao?

    Kimsingi kosa alilonalo Makonda linaweza kuwa kubwa kwani linagusa maisha lakini linakosa mashiko kutona na muda lilipoibuliwa. Kweli tulisubiri wauza unga watajwe ndo tumsaidie rais kuchunguza elimu ya Makonda?

    Binafsi ninavyoona mimi wanaotaka Makonda atumbuliwe si wazalendo bali ni wa maslahi binafsi na wanaotaka kulipa kisasi pindi huyu jamaa atakaporudi mtaani. Ashukuriwe Mungu Mh. Rais kaliona hilo.

    ReplyDelete

Top Post Ad