Baada ya Kumpa Makavu Diamond...Erick Shigongo Amgeukia Ali Kiba na Kusema Haya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baada ya kumshauri Diamond leo nataka nimshauri Ali Kiba. Sijui kama atafurahi au atachukia, ninafanya hivi kwa kuwa sitaki waache muziki hapo baadaye huku wakiwa hawana kitu. Sitaki baadaye mtu aseme kwamba kuna watu waliwatumia, wakaingiza pesa halafu wamewakimbia.
Baada ya kusema hayo hebu niongee kilichonisukuma kuandika hiki ninachokiandika, ni ushauri, Kiba na meneja wake wanaweza kuuchukua ama kuuacha! Si lazima, kama mhamasishaji wa watu kujiondoa katika umasikini ninaona kama ninao wajibu wa kumshauri Kiba nikiwa kama kaka, anko au Mtanzania mwenzake, naamini kwa hekima walizonazo Ali Kiba na meneja wake bila shaka watapata la kuchukua, yasiyofaa wataniachia mwenyewe.
Nampenda Kiba sana tu na ninajivuna sana kuwa Mtanzania mwenzake na ningependa kuona anafanikiwa zaidi katika kazi yake. Kama siwezi kufurahi mafanikio ya Watanzania wenzangu basi hakuna haja ya mimi kuzunguka huku na kule ndani na nje ya nchi yangu kuhubiri injili ya mafanikio, watu watoke kwenye umasikini unaolitesa taifa langu.
Haikutokea tu Ali kiba akawa anapendwa vile, la hasha, ni matokeo ya vitendo fulani ambavyo amekuwa akivifanya maishani mwake mpaka Akawavuta watu kumpenda! Mambo hayo hayo akiyaacha hata followers wa Instagram wanaomfanya ajisikie anapendwa leo wataondoka!
Ali kiba, meneja wake na Watanzania wenzangu lazima mnisikilize hapa; MAFANIKIO MAISHANI HUJA NA KITU NYUMA YAKE, mara nyingi kitu hicho huwa kuwapuuza na kuwadharau waliokufikisha ulipo. Kuwatenga bila kufahamu hao ndiyo wanunuzi wa kazi zako ama wasikilizaji wa muziki wako na wakikuachia tu utatumbukia shimoni na huo ndiyo utakuwap mwisho wako.
Ali kiba anapaswa kufahamu kwamba hawezi kuwa Champion for life, hata akiwa bora kiasi gani lazima siku moja atakuja mtu bora zaidi yake. Kabla ya Chris Brown alikuwepo Usher Raymond, kabla ya Rihanna alikuwepo Beyoncé, kabla ya Floyd Maywether alikuwepo Mike Tyson, kila zama na bingwa wake. Leo ni Kiba kesho atakuwa mwingine, swali la kujiuliza ni kwamba: SIKU ALI KIBAm ATAKAPOKUWA NJE NANI ATABAKI NAYE?
Inaendelea post inayofuata...
.
JE, UMEMUELEWA SHIGONGO??? TOA MAONI YAKO HAPA
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad