Jakaya Kikwete Kiongozi Bora Aliyeandamwa na Kukosolewa kwa Hila na Chuki..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Jakaya kikwete alikuwa kiongozi wa nchi yetu aliyejitahidi sana kutoa uongozi bora unaozingatia sheria za nchi na kuleta maendeleo katika nchi yetu .

Alijitahidi sana kuboresha hali za maisha ya watu kwa kuongeza kipato na kutengeneza mazingira mazuri ya biashara .

Aliongeza stahiki kwa watumishi wa umma na kuwafanya wakopesheke kwa ajili ya maendeleo .
Aliongeza upatikanaji wa umeme na maji kote nchini hadi vijijini .

Alihakikisha kila mtu anapata fursa ya kusoma kadri ya uwezo wake .
Tukashuhudia maendeleo makubwa katika Huduma za afya na miundombinu kuanzia barabara hadi viwanja vya ndege .

Itoshe tuu kusema alifanya mengi mazuri ya kupigiwa mfano kwa nchi yetu .

Ni kweli yalikuwepo mapungufu mengi katika utawala wake lakini Mapungufu yalikuzwa mazuri yakadhoofishwa .

Juhudi kubwa zilifanywa kuonesha kuwa ni kiongozi asiyefaa hata kidogo na aina yake ya utawala nayo haifai .

Hila na chuki zikapandikizwa juu yake .
Nyumba za ibada zikatumika kumdhoofisha na kudhoofisha utawala wake .
Tukashuhudia manyaraka yakitolewa kila mara kuikosoa na kuikaripia serikali yake ?
Leo najiuliza Nyaraka zile ziko wapi kama kweli walikuwa wanafanya vile kwa dhamira njema na uzalendo kwa nchi ?

Hakuna Kingine isipokuwa walikuwa wanafanya vile kwa hila na chuki .
Ndio maana ukosoaji wao una msimu .

Nakumbuka wakati anaaga ccm alisema "Historia itatoa hukumu iliyo ya haki ".

Leo waliokuwa wanambeza na kumkashifu sasa wanaongoza kumsifu na kumpongeza .

Ili tujenge nchi yetu ni lazima kuwa wazalendo na kuepuka hila na chuki .

Tunawajibu wa kuwakosoa viongozi wetu lakini tusifanye hivyo kwa hila na chuki tufanye hivyo kwa dhamira njema na mapenzi kwa nchi yetu .

" Tukipanda mbegu za hila na chuki tutavuna matunda ya hila na chuki ".
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na ule ufisadi wa mabilioni.kupelekea kuyumba kwa kila nyanja. mahospitali vifaa bua kina mama kujifungulia hkuna.huduma nzuri tabu.dawa hakuna wagonjwa kulala chini. vijimiundo mbinu vichache tu. na nyie mafisadi papa ambao wengine kina siku iendayo wanaondoka na mamilioni hamsini. nani asiejua na way tunaishi nao. msituchoshe sei watu wa kawaida.na walala hoi. nyie wandishi uchwala.Na nadhani wasomaji wa humu ni like kundi la Elimu ya kayumba. ili wawapotoshe hebu tutoleeni kule.

    ReplyDelete
  2. wambiage hao hao wajinga sawa weee. wandishi uchwalaa😴au waliolala zzzz. icho kiwanja chenyewe cha ndege kilitakiwa kiwe kikubwa lakini mahela yakapagwa mengi na kijiwanja cha ndege kidogo.mahela yalikuwa yapigwe panga. Na mtoaji ni wa sasa. kikiisha awape mahela yao. huyu yuko makini kuona hicho kiwanja michosho mmmmh akashitukaa. sasa hatutaki habari za kusikia mara yule mara hivi. eti kwa faida za wachache. wanaowaibia wenzao kila kukuchaa. Ndio maana Africa haiendelei kwa khali kama hizi ni ndoto bara la Africa kusonga mbele. mafisadi ni Kama utamaduni wao.

    ReplyDelete
  3. wambiage hao hao wajinga sawa weee. wandishi uchwalaa😴au waliolala zzzz. icho kiwanja chenyewe cha ndege kilitakiwa kiwe kikubwa lakini mahela yakapagwa mengi na kijiwanja cha ndege kidogo.mahela yalikuwa yapigwe panga. Na mtoaji ni wa sasa. kikiisha awape mahela yao. huyu yuko makini kuona hicho kiwanja michosho mmmmh akashitukaa. sasa hatutaki habari za kusikia mara yule mara hivi. eti kwa faida za wachache. wanaowaibia wenzao kila kukuchaa. Ndio maana Africa haiendelei kwa khali kama hizi ni ndoto bara la Africa kusonga mbele. mafisadi ni Kama utamaduni wao.

    ReplyDelete
  4. Usisahau na kuongelea habari ya unyanyasaji na wizi tuliofanyiwa sie maskini. Haki yako mwenyewe utazulumiwa na mwenye hela za kuhonga. Huduma za serikali hupati bila hongo. Hongo ikalazimishwa kwa kila ulifanyalo bila kutoa hakuna ulipatalo. Nchi ikawa ya watu fulani na fulani.

    ReplyDelete

Top Post Ad