Kimenukaaa...Bunge, Maalim Seif Wambana Msajili Kuhusu Mgogoro wa CUF..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wakati katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif akisema kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi anakivuruga chama chao, Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba imemtaka kuhakikisha anamaliza mgogoro wa chama hicho kuepusha kutia dosari Muungano.

Kauli hizo zimekuja siku moja baada ya Bunge kumtambua naibu katibu mkuu wa CUF-Bara, Magdalena Sakaya kuwa kaimu katibu wa chama hicho kwa maelezo kuwa Maalim Seif anashindwa kutekeleza majukumu yake.

Bunge lilifikia uamuzi wa kutambua pande zote zinazopingana kwenye mgogoro huo baada ya Msajili kumwandikia Profesa Ibrahim Lipumba kumweleza kuwa amekubali ombi lake la kutaka Sakaya atambuliwe kama kaimu katibu mkuu, jambo ambalo linaonekana kuzidi kukigawa chama hicho.

Profesa Lipumba aliingia kwenye mgogoro na chama chake baada ya kuandika barua ya kujivua uenyekiti na kukaa nje kwa takriban mwaka mmoja kabla ya kurejea nchini na kuandika barua ya kufuta uamuzi wa kujiuzulu uenyekiti, jambo ambalo mkutano mkuu wa CUF ulilikataa na kuridhia kujiuzulu kwake.

Mgogoro huo umefanya kuwa na pande mbili; wa kwanza ukikubaliana na uamuzi wa mkutano mkuu wa kuridhia kujiuzulu kwa Lipumba, na wa pili ukikubaliana na kujirejesha madarakani kwa msomi huyo.

Upande wa kwanza unaendesha shughuli zake kutoka makao makuu ya CUF yaliyopo kisiwani Unguja na wa pili ukiwa ofisi kuu zilizopo Buguruni jijini Dar es Salaam.

Jana, kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ilimtaka Jaji Mutungi kuchukua jitihada za kuumaliza mgogoro wa CUF ili kuepusha athari kubwa zinazoweza kujitokeza katika Muungano.

Akisoma maoni ya kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka wa 2016/17 na ile ya 2017/18, mjumbe wa kamati hiyo, Joseph Mhagama alisema mgogoro huo unaweza kusababisha athari za Muungano.

“Katika mgogoro unaoendelea ndani ya CUF, Kamati inashauri Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuchukua jitihada za kutosha kusuluhisha mgogoro huo ili kuepusha athari kubwa zinazoweza kujitokeza katika Muungano,” alisema.

Mhagama alisema kamati hiyo inaiagiza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na weledi katika kusimamia na utoaji wa ruzuku kwa vyama vya siasa na kuhakikisha kwamba taratibu hizo zinafuatwa katika utoaji ruzuku kwa vyama vya siasa.

Wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani na madiwani, Msajili alitoa ruzuku ya zaidi ya Sh300 milioni ambazo zilichukuliwa na upande wa Profesa Lipumba ambao ulibadilisha majina ya watia saini wa akaunti iliyokuwa wilayani Temeke.

Oktoba mwaka jana, Bodi ya Wadhamini ya CUF ilifungua kesi Mahakama Kuu dhidi ya Msajili, Profesa Lipumba na wanachama 12 waliosimamishwa. Pamoja na mambo mengine, bodi hiyo inataka Msajili.

Katika kesi hiyo, bodi inaiomba mahakama ibatilishe barua ya Msajili ya Septem,ba 23 mwaka jana iliyotengua uamuzi wa Mkutano Mkuu wa kukubali kujiuzulu kwa Profesa Lipumba, imzuie Msajili asiendelee kufuatilia suala la kufutwa kwa uanachama wa Profesa Lipumba na pia azuiwe kuingilia mambo ya CUF.

Jana akizungumza na gazeti hili kuhusu uamuzi wa Msajili kumtambua rasmi Sakaya kukaimu nafasi yake, Maalim Seif aalisema Jaji Mutungi ndiye chanzo cha matatizo ya chama hicho.

Alisema Profesa Lipumba si mwanachama wa CUF na pia si mwenyekiti wao kama anavyotambuliwa na Msajili.

“Tangu mwanzo Msajili aliamua kuchukua upande na kuwa pamoja na Lipumba na ndiye mshauri wake. Wanashauriana kwa kila hali, lakini bado ukweli unabaki pale pale kwamba Lipumba si mwanachama kwa mujibu wa katiba ya CUF,” alisema Maalim Seif.

Maalim Seif alisema hata kama Profesa Lipumba angekuwa ni mwenyekiti, hana uwezo kumuengua katibu mkuu wa CUF.

“Chombo ambacho kina uwezo wa kuwashughulikia na kumsimamisha mwenyekiti, makamu mwenyekiti au katibu mkuu ni Baraza Kuu la Uongozi la Taifa. Halafu kama kuna kesi wanapeleka mkutano mkuu ambao unafanya maamuzi,” alisema Maalim Seif.

“Hata huyo Magdalena Sakaya mwenyewe naye kasimamishwa uanachama, si mwanachama. Mutungi ndiye anaendelea kulivuruga suala hili kwa mapenzi yake kwa Lipumba au sijui anapata instruction (maelekezo), sijui. Lakini Lipumba si mwenyekiti wetu, si mwanachama wa CUF.”

Alisema uchaguzi wa wabunge wa Eala umeharibika kwa sababu ya Msajili kukubali waliowapendekezwa na Lipumba ambao si wanachama.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Jumanne, Maalim Seif alipeleka jina la mgombea mmoja, wakati upande wa Lipumba ulipeleka majina matatu na ofisi ya Bunge ikayapokea yote, ikiyaweka majina hayo chini ya CUF “A” na CUF “B” kwa kuzingatia maelekezo ya Msajili.

Maalim Seif alisema Habib Mnyaa, ambaye alichaguliwa kuwa mbunge wa Eala baada ya jina lake kuwasilishwa na Sakaya, alifukuzwa uanachama na tawi lake na katiba yao inasema hawezi kurudi uanachama hadi miaka miwili ipite.

“Yote haya Mutungi ndiyo kayachukua yeye ndiyo anavuruga na anaendelea kuvuruga,” alisema.

Jana, Jaji Mutungi alisema hatazungumzia suala hilo tena na vyombo vya habari, ma kumtaka Maalim Seif asubiri uamuzi wa mahakama.

“Waandishi wa habari acheni kuendesha debate (mjadala) kuhusu suala hili kwa sababu liko mahakamani,” alisema Jaji Mutungi.

Jaji Mutungi ametoa onyo hilo wakati ameshtakiwa mahakamani lakini ofisi yake ikimwandikia barua Profesa Lipumba kukubali uteuzi wake wa Sakaya kuwa kaimu katibu mkuu.

Barua hiyo ya Machi 21 imesainiwa na Sisty Nyahoza wa ofisi ya Msajili na inamweleza Profesa Lipumba kuwa itampa ushirikiano Sakaya katika majukumu yake ya kukaimu nafasi ya katibu mkuu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad