Kimenukaa..Mama Samia Suluhu Hassan Awaumbua Kina Mange Kimambi na Genge Lake..Afunguka Haya Kuhusu Uwekezaji Nchini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa Tanzania ni moja ya nchi salama kwa uwekezaji Afrika.

Amesema hilo linasababishwa na kutokuwa na matatizo ya migogoro ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa mali za wawekezaji ikilinganishwa na nchi zingine Afrika.

Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua maonesho ya kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania yanayofanyika Dar es Salaam.

Pia alikaribisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Ufaransa kuwekeza katika maeneo mbalimbali hasa kwenye kilimo, nishati, utalii na usafiri kutokana na hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.

Makamu wa Rais alisema maonesho hayo ambayo yataambatana na kongamano la kibiashara la nchi hizo mbili ni fursa ya kipekee kwa wafanyabishara wa Tanzania na Ufaransa kubadilishana uzoefu katika masuala ya kibiashara na uwekezaji.

Alieleza kuwa katika kuelekea kwenye uchumi wa viwanda Tanzania haiwezi kufanya kazi hiyo peke yake, bali kwa kushirikiana na mataifa makubwa yenye teknolojia ya kisasa katika uwekezaji ikiwamo Ufaransa.

Aliwahakikishia wawekezaji wote wanaokuja nchini kuwa Serikali itafanya kila linalowezekana kuendelea kujenga mazingira bora kwa ajili ya uwekezaji.

Alisema ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na mazingira bora ya uwekezaji Afrika, Serikali imeendelea kutenga bajeti ya kutosha kuimarisha miundombinu ya bandari, reli, barabara, usafiri wa anga ili kurahisisha usafiri na usafirishaji nchini.

Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema kongamano hilo litajikita katika kujadili kwa kina fursa za uwekezaji nchini hasa kwenye nishati, usafirishaji, teknolojia ya habari na mawasiliano na miradi ya maendeleo.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram,Mara Kadhaa Mwanadada Mange Kimambi Amekuwa Akidai kuwa Tanzania si Sehemu Salama kwa Uwekezaji kutokana naAina ya Serikali Iliyopo hivi sasas.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania kweli kwa sasa si Nchi ya kuwekeza kulingana na uonhozi wa Serikali ya awamu ya tano ilivyo ni matamko kila iitwapo leo yasiyojenga vijembe kama waimba taarabu naungana na Kinambi

    ReplyDelete
  2. Mama Samia, Tunawatanzania wengi wanapenda kilimo, vijana, kinamama. Hakuna haja kwenda Ufaransa kuwaleta Wazungu nchini. Naona Aibu. Serikali inabidi iwasaidie Watanzania hasa Vijana iwaunganishe na iwapo nyenzo na ushirikiano. Unamhitaji mtaalamu moja au wawili tu.Kwa nini mnawaleta Wakoloni nchini na kwatengenezea mazingira mazuri kiuwekezaji na kumtupa Mtanzania anayetaka kujiajili. Mbona hamna ubunifu mzuri na ushirikiano na Watanzania nchini. Kuna nini viongozi wa juu wa serikali ya CCM? Mnaiumiza nchi yetu, mnaigawa nchi na Watu, Mnawathamini wawekezaji dhidi ya Watanzania.
    Am ashamed and something wrong, very wrong.

    ReplyDelete

Top Post Ad