Kudadeki..Umesikia Hii Kuhusu Yanga...?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KOCHA msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema kuongezeka kwa majeruhi katika kikosi chao ni pigo na wataivaa kiugumu MC Alger ya Algeria katika mchezo wa Kombe la barani Afrika utakaochezwa wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kikosi cha Yanga kinakabiliwa na majeruhi wengi baada ya Mzambia Justine Zullu kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam uliochezwa juzi, Uwanja wa Taifa na wao kushinda bao 1-0.

Wachezaji wengine majeruhi ni  washambuliaji Amis Tambwe, Donald Ngoma, kiungo Thabani Kamusoko na  beki Pato Ngonyani.

Akizungumza  juzi, Mwambusi alisema majeruhi walionao wamezidi kupunguza idadi ya wachezaji muhimu wa kikosi chao cha  kwanza.

Mwambusi alisema hali hiyo imekuwa ikiwagharimu mara nyingi ukizingatia wameanza vibaya katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa mapema.

“Inasikitisha sana kuongezeka kwa majeruhi katika kikosi chetu, tunazidi kuwapunguza watu na tunakwenda kwenye michuano muhimu ambayo lengo letu ni kufanya vizuri baada ya kuanza vibaya,” alisema Mwambusi.

Mwambusi alisema malengo yao ni kutaka kufika mbali katika michuano hiyo, lakini wamekuwa wakiandamwa na majeraha na ni pigo.

Alisema wachezaji watano majeruhi ambao wanacheza kikosi cha kwanza, hivyo wanahitaji kufanya kazi kubwa  kurudi katika hali ya kawaida.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad