PATA Hii...Nyoka ni Marafiki Zetu na Sio Maadui, Tusiwadhuru Bila ya Sababu Bali Tujenge Nao Urafiki..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ndugu zanguni kuna tabia ambayo imezoeleka miongoni mwa wengi kila waonapo nyoka wanawapiga na mawe,magongo na silaha aina yeyote ile mpaka wanawaua hata pale nyoka akiwa sehemu pekee yake ametulia bila bughudha yeyote ile ila utashangaa mtu anaanza kupiga yowe na kuita kadamnasi ya watu na kisha kumshambulia nyoka ambaye alikuwa amejituliza zake tu.

Kwanini tunawachukia kwa kiasi kikubwa nyoka?

Watu wanadai Nyoka ni adui ya binaadamu lakini tusisahau sisi ndio tunaojenga uadui nao sababu kila tukiwaona tunaanza kuwashambulia hata kama hawakuwa na kosa ya aina yeyote ile

Mfano hawa nyoka wa majumbani green snake au black snake ambao kipindi cha baridi hukimbilia majumbani kwa watu kutafuta joto.

Nakumbuka nilivyokuwa mdogo maeneo ya Mbeya hawa nyoka walikuwa na tabia ya kuingia ndani kutafuta joto na hawakuwa na nia yeyote ile mbaya lakini cha kushangaza huyo nyoka akionekana watu huanza kupiga yowe na kisha anauliwa kikatili badala ya kupewa msaada wa joto,anakimbia shida na anakutana na dhahma.

Ili kuthibitisha nyoka ni marafiki zetu na sio maadui wetu nadhani wengi ni mashahidi kuna wakati nyoka akikimbia baridi na kutafuta hifadhi yenye joto hukimbilia majumbani na wakati mwingine hujibanza karibu na mtu ,wangapi wanalala na nyoka bila ya kujijua?na wengine wakishafahamu wamelala na nyoka wakistuka wanaanza kupiga yowe kisha kumuua nyoka huyo.Inashangaza sana huyo nyoka angetaka kukudhuru basi angekudhuru kitambo sana kwani hajui kama amejibanza karibu na mtu?

Kwani harufu ya mtu haifahamu lakini kutokana hakubughudhiwa na yeye shida yake ni joto hivyo ameamua kujisogeza karibu na shuka apate joto akishapumzika anakwenda zake..lakini sie tunachowafanyia sio haki kabisa 

Pia ni kesi ngapi tunashuhudia watoto wadogo wakicheza na nyoka tena muda mrefu bila kudhuriwa ,sababu haswa nyoka sio adui na mtoto hajui kudhuru 

Kwa hizi sababu mbili tufahamu nyoka ni rafiki na sio adui lakini rafiki maisha yake yakiwa hatarini lazima ajilinde na njia sahihi ya kujilinda ni kushambulia

Nawasihi ndugu zangu sio kila tukimuona nyoka tunapiga mayowe na kuanza kutafuta mawe,fimbo na kuanza kuwashambulia ,sisi ndio tunawafanya wakasirike lakini nyoka ni marafiki haswa nyoka wa majumbani hawa na pale wakitafuta hifadhi ya joto tusiwadhuru 

Mie hawa nyoka wamenisaidia sana kunisafishia shamba na nyumba ,wadudu kama mende ,panya na aina wafananao wameisha sababu ya hawa home snakes wana msaada sana.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwandishi utakua mchawi sio bure, kweli umuone nyoka ndani umchekelee tu, kawa mjombako?

    ReplyDelete
  2. Huyu atakuwa kizazi cha nyoka sio bure. Unatokwa povu jingi kutetea nyoka?? Maandiko matakatifu yameweka wazi mahusiano ya mwanadamu na nyoka. Usitake kutulisha ufahamu wako haba. Soma kwanza kisha ufundishe

    ReplyDelete

Top Post Ad