RASMI..Cuf ya Lipumba Wafunguka Sababu Hizi za Kuvamia na Kufanya Vurugu Kwenye Mkutano wa Maalim Seif

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Siku chache zilizopita baada ya kutokea fujo kwenye mkutano wa CUF uliokuwa umeandaliwa na upande wa wafuasi wa Maalim Seif Sharif Hamad, upande wa pili umejitokeza na kukiri hadharani kuwa vijana waliofanya fujo katika mkutano huo walikuwa ni wa CUF.

Hayo yamesemwa mapema hii jana Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Buguruni Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdul Kambaya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema vijana waliofanya fujo kwenye mkutano huo walikuwa ni Chama hicho.

Amesema kuwa vijana walikuwa katika doria la kawaida kwani tayari walikuwa wameshapata taarifa za mkutano huo ambao haukutakiwa kufanyika mujibu wa katiba ya chama hicho.

“Mtu yeyote asipindishe kitu, wale hawakuwa majabazi, ni vijana wetu wa CUF na walikuwa kwenye doria kwa sababu tulishasikia mikakati yao wanayoipanga na Chadema, hatuwezi kupangiwa mipango na Ukawa wakati sisi ni Chama halali,”amesema Kambaya.

Aidha, Kambaya ameongeza kuwa mchezo mchafu anaoucheza Meya wa Ubungo, Boniface Jacob na Chadema kwa ujumla wa kutaka kuisambaratisha CUF hautafanikiwa.

Hata hivyo, katika hatua nyingine, Kambaya amesema kuwa Chama Cha Wananchi (CUF),kinaomba radhi kwa waandishi wa habari, Jukwaa la Wahariri pamoja na vyombo vyao kwa tukio hilo lililolsababisha taharuki kubwa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad