CCM Arusha Wamjibu Lowassa Sakata la Msiba wa Wanafunzi Lucky Vicent..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha kimeishangaa kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kusema kuwa Rais John Magufuli amemtuma ‘mtoto mdogo’ kwenda kuiwakilisha serikali kwenye mazishi ya wanafunzi wa  shule ya Lucky Vicent

 Akizungumza  na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Michael Lekule ,amesema kauli ya Waziri huyo mstaafu ameitoa kwa kudanganya wananchi na kuonesha serikali ya Magufuli haishirikiani na wananchi ,wakati serikali iliubeba msiba huo mzito wa taifa.

 Amesema jitihada za serikali ya Magufuli zimeonekana kupitia kwa wawakilishi wake Makamu wa Rais Samia Suluhu pamoja na Mrisho Gambo pamoja na wanachama wa CCM ambao walijitokeza kwa wingi kwenye msiba huo mzito

 "Serikali ilijitoa kwa hali na mali kuwezesha  familia 35 kwenda kupumzisha wapendwa wao,na ilihakikisha kila mwili unapumzika mahala popote familia inapopata,tunajiuliza walitaka nini kama kote nafasi ilijazwa na serikali ya Magufuli," alisema Michael

 "CCM inakanusha kwanguvu upotoshaji huo,hata ukiangalia siku ile uwanja wa shekh Amri Abeid wanaccm walijaa uwanjani ,kikubwa CCM imeguswa na msiba uliotokea na Rais wetu amekuwa bega kwa bega juu ya tukio lililotokea,"amesema

 Pia amesema wamemshangaa kwa kusema Rais alimtuma mtoto mdogo wakati yeye mwaka 2007 ajali mbaya iliyotokea Monduli duka bovu na kuua watu 20 ambao 11 walikuwa ni askari wa JKT,rais Kikwete alimtuma aje kuiwakilisha serikali.

 Hata hivyo alimtaka kiongozi huyo, ajiulize kama yeye kipindi akiwa Waziri Mkuu aliweza kutumwa na Rais, amuwakilishe kwenye msiba wa watu 20, je yeye na Makamu wa Rais ni nani mdogo?

 "Tena ajali hiyo ilikuwa ya kitaifa,askari 11 walifariki kwenye ajali,mbona hajayasema ya kwake?," amesema Lekule
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Siasa ni siasa. Na siasa ni mbinu chafu. Itafika siku Watanzania baada ya kukitetea Chama chao kwanza, watafute maslahi ya Watanzania kwanza waliowachagua na wanaowalipa mishahara. Lakini papo hapo Kimwamko kifikra Watanzania wa leo wameshuka sana.Zamani mjumbe kumi alikuwa na utu, hedhima, na kugombania maslahi ya watu. Sasa ni nembo ya matumbo tu. Sababu wengi si wazalendo, elimu duni, na kutokujitambua kwamba elimu zao ni duni, ni Tatizo kwa nchi nzima.
    Nchi haina mwelekeo mzuri, ingawa kuna Wachache wanajitahidi sana kuirudisha nchi kati. Sheria hazifuatwi, bali kauli zinafuatwa. Watanzania inabidi tufundishwe elimu na kuzijua sheria zetu. Ni hivi tu tatatambua nchi iko gizani.

    ReplyDelete

Top Post Ad