Masikini Prof Muhongo..Hivi Ndivyo Safari Yake ya Uwaziri Ilivyokuwa na Misukosuko kama Meli Baharini..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amepitia misukosuko katika nafasi za uwaziri tangu alipoteuliwa na Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

 Jana Rais John Magufuli alimtaka Profesa Muhongo ajitathmini kuhusu nafasi yake ya Uwaziri baada ya kupokea ripoti ya mchanga wa madini Ikulu.

Mei 2012, Rais Kikwete alimteua Muhongo kuwa mbunge pamoja na wabunge wengine watatu, akiwamo Janet Mbene na James Mbatia.

Baada ya kuteuliwa na kuwa mbunge, Muhongo aliteuliwa na kuwa Waziri wa Nishati na Madini  na Rais Kikwete.

Hata hivyo Januari 24 mwaka 2015, alimuandikia Rais barua ya kujiuzulu kutokana na sakata la uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Mwaka mmoja baadaye, baada ya Rais John Magufuli kuingia madarakani, alimteua tena Profesa Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Muhongo alishinda kiti cha ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini kwa tiketi ya CCM, katika uchaguzi wa 2015.

Lakini jana tena, ikiwa ni miaka zaidi ya miwili tangu ajiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow, ametakiwa kujiuzulu kutokana na  sakata la mchanga wa madini.muda mfupi baada ya kutakiwa ajitathimini akapokea barua ya kutenguliwa uwaziri


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad