MBUNGE Amwaga Chozi Bungeni..Kisa Ni..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Faida Bakari amemwaga chozi bungeni akielezea udhalilishaji unaofanywa kwa watoto nchini.

Faida akichangia bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2017/18 bungeni leo mjini Dodoma amesema watoto wanadhalilishwa kwa kufanyiwa vitendo vibaya na watu wazima. Ameiomba Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wanaobainika kufanya hivyo.

“Watoto wanaharibiwa mheshimiwa waziri, naomba mchukue hatua kali za kisheria kwa watu hawa. Nilienda Pemba nililia watoto wanaharibiwa maumbo. Mheshimiwa nasema kwa uchungu,” anasema huku akilia na kuvuta pumzi ndefu kabla ya kuendelea kuzungumza.

Anasema walimu wamekuwa wakiwadhalilisha watoto huko Pemba na kumuomba waziri ashughulikie suala hilo.

“Tumrudie Mungu, unakuta mibaba mizima inawapa mimba watoto na madevu yao mengi wanawatia watoto wenzao mimba,” anasema.

Faida pia amesema wazee wamekuwa wakinyanyaswa katika jamii na kuwataka Watanzania kuwatunza kwa sababu ipo siku nao watakuwa wazee. “Ukiona nyumba zao unalia naomba  mheshimiwa uangalie katika eneo hili la wazee.”

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Suzan Lyimo yeye alisema wazee wametelekezwa katika kambi za kuwahudumia na kuitaka Serikali kuwaangalia.

“Mwaka jana mlisema mtaleta Sheria ya Wazee lakini mwaka huu haikuzungumzwa, hakuna sheria ya wazazi ndiyo maana wazee bado wanauawa,” alisema.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad