Mtoto Akatwa Makalio na Baba ake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanamume mmoja mkazi wa Ndofe wilayani Nyamagana mkoani Mwanza amemfanyia kitendo cha ukatili mtoto wake kwa kumkata na kisu sehemu za makalio kwa madai ya utoro shuleni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Nuhu James (50) anayedaiwa kumfanyia ukatili mtoto Ndalo Nuhu (14) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Igoma kwa kumfunga kamba miguuni na mikononi kisha kumchapa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baadaye kumkata na kisu sehemu za makalio, tukio analodaiwa kulifanya majira ya saa 11:00 alfajiri ya tarehe 25 Mei, 2017.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa aliaamua kumfanyia ukatili wa aina hiyo mtoto wake baada ya kugundua kwamba mwanaye ni mtoro shuleni.

Kamanda Msangi amesema baada ya mama wa mtoto alipoona ukatili anaofanyiwa mwanaye na hali yake kiafya kuzidi kubadilika alishindwa kuvumilia na jana (Tarehe 28 Mei.2017) aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi

Kamanda Msangi ameendelea kusema kuwa polisi wapo katika upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi utakapokamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani huku majeruhi akipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad