POLISI: Mauaji ya Kibiti, Rufiji Hayajapoteza Amani..!!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KAMISHNA wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania, Nsato Mssanzya, amesema matukio ya uhalifu yanayoendelea maeneo mbalimbali nchini, hasa Kibiti na Rufiji yasitafsiriwe kuwa Taifa limepoteza amani.

Aidha, amesema watu wanaouawa wasihusishwe na vyama vya siasa, kwani hakuna taarifa zinazoonesha kuuawa kutokana na vyama vyao, kwani matukio ya uhalifu yako duniani kote.

Mssanzya  alisema Jeshi la Polisi limejipanga kila kona kuhakikisha amani inadumu nchini, akieleza kwamba matukio yanayotokea si taswira sahihi ya kusema Taifa halina amani.

“Kila siku inayopita ni vigumu kutopata taarifa ya matukio ya uhalifu, hivyo hali hiyo isihusishwe na kukosekana kwa amani nchini, lakini pia si vema kuhusisha matukio hayo na siasa,” alisema.

Kamishna alisema hali ya usalama ni nzuri na hakuna mwananchi anayekosa amani.

Alisema wananchi katika maeneo yanayotajwa kuwa na uhalifu wananchi wanajihusisha na shughuli za uzalishaji hali aliyosema inatoa tafsiri ya uwepo wa amani.

Hata hivyo, alisema Jeshi hilo limejipanga kupambana na uhalifu bila kuangalia siasa au vyama, kwani wanaopoteza maisha ni raia wa Tanzania.

Alisema yanayotokea Kibiti na Rufiji ni matukio kama mengine na kinachotakiwa ni wananchi kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu na matukio hayo kwa Jeshi hilo, ili liweze kuyafanyia kazi haraka.

Kamishna alisema matukio mengi yanayotokea Kibiti na Rufiji yamekuwa yakitokea vijijini, ambako hakuna polisi tofauti na ilivyo mijini na kwamba kinachohitajika ni taarifa za haraka.

Kamishna aliwataka wananchi kushirikiana na Jeshi hilo kufanikisha kukamata wahusika, ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad