TANZANIA Kununua Ndege nyingine Mpya Mwezi wa 7 Mwaka Huu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali iko kwenye mpango wa kuongeza  ndege nyingine moja ili zizidi kufika sehemu nyingi zaidi Tanzania ambapo Naibu Waziri wa wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani  amesema July 2017 ndio inanunuliwa nyingine.

Amesema Ndege hiyo itakayonunuliwa July ni aina ya Dash 8-Q 400 ambapo hatua hiyo italifanya shirika la ATCL kufikisha Ndege nne (4) ambazo zitaongeza safari zake kwa kuhudumia masoko yake ya ndani na miji ya Nchi jirani kama vile Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).

Ni kauli ambayo aliitoa wakati wa uzinduzi wa safari za Ndege za ATCL kwenye mkoa Tabora na kuongezea kwamba lengo la Serikali ni kuhakikisha hadi kufikia July 2018 Shirika la Ndege Tanzania liwe linamiliki Ndege sita zenye uwezo wa kubeba abiria kwa kiwango tofauti tofauti na kusafiri mikoa mingi na nje ya Tanzania.

Naibu Waziri alisema hadi sasa Serikali imeshanunua ndege mbili aina ya Bombardier Dash 8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na hatua inayofuata ni ununuzi wa ndege nyingine tatu aina ya Bombardier Dash 8-Q400 yenye uwezo kubeba abiria 76, CS 300 mbili zitakazobeba abiria 132 kila moja na Boeing 787 ya kubeba abiria 262.

Alisema kuwa hatua hiyo inaenda sambamba na uimarishaji wa Shirika la Ndege hapa nchini na ujenzi wa viwanja vipya vya ndege katika mikoa ambayo haina viwanja hivyo kwa sasa ili ifike siku mikoa yote Tanzania iweze kuunganishwa na usafiri wa anga
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mungu ibariki Tanzania yetu, wabariki viongozi wake na watu wake.

    ReplyDelete

Top Post Ad