WABUNGE Wafichua Mazingaombwe Kwenye Vitabu vya Shule za Msingi..!!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wabunge ‘wamewaka’ kuhusu makosa yaliyopo kwenye vitabu vya kujifunzia na kushauri kuzuia matumizi ya vitabu hivyo ili kuepuka kuendelea kuwaharibu wanafunzi shuleni.

Makosa yaliyobainika katika vitabu hivyo ni ya kisarufi, mpangilio wa kurasa, tafsiri sisisi na kimantiki.

Wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2017/18 bungeni mjini Dodoma jana, walisema vitabu hivyo vina makosa mengi ya lugha ya Kiswahili na Kingereza jambo ambalo linaua elimu nchini.

Akisoma maoni ya kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Suzan Lyimo alisema pia makosa hayo yamekithiri katika herufi kubwa na ndogo na matumizi ya nukta pacha. “Matatizo hayo yamo kwenye vitabu vyote hasa kujifunza kusoma, kuandika, kuhesabu, afya na mazingira, michezo na sanaa,” alisema.

Alitoa mfano wa Kitabu cha Najifunza Kusoma, darasa la Kwanza, ukurasa wa 99 kinataja kucha kikimaanisha ukucha. Pia kitabu hicho kinaeleza kumjulisha bila kubadili kwa wima (baada ya kumjumulisha kwa wima bila kubadili) ukurasa 93 na 94 maneno chupa/ chupa ya chai (yakichanganywa).

Lyimo alisema kitabu cha I Learn English Language, kina matatizo ya matumizi ya herufi kubwa na ndogo mengi mno karibuni kila ukurasa.

“Inaelekea pia mwandishi hana uwezo wa kutosha wa lugha yenyewe kwani kuna makosa mengi.”

Alitoa mfano wa sentensi ambazo zimekosewa kuwa ni These are my parent, which is long between a pen and ruler? The driver is taken the police station, a boy is on bed at hospital na which is the big city of Tanzania (meaning Capital City).

“Vitabu vya darasa la kwanza vilichelewa kuchapishwa na kuwasilishwa shuleni. Hata hivyo, baada ya hekaheka nyingi za kuchoma nakala zilizokuwa na makosa ya mchapishaji, baadhi ya vitabu vya darasa la kwanza vilitoka Juni, 2016 na baadhi ya Januari mwaka 2017,” alisema.

Alisema kitabu kimoja tu cha darasa la pili kimetoka mwaka huu wa 2017 na kingine cha Kingereza darasa la tatu, I learn English Language.

“Kwa hali hiyo ya utoaji wa vitabu vipya na ucheleweshaji, walimu na wanafunzi watapata shida kubwa kuutumia mtaala mpya,” alisema.

Lyimo aliitaka Serikali kuzuia matumizi ya vitabu hivyo vyenye makosa shuleni na pia kuiagiza taasisi elimu kufanya marekebisho ya makosa yaliyopo kwenye vitabu hivyo na kuvichapisha upya.

Aidha, aliitaka Serikali kufanya uhakiki wa taaluma na weledi wa watumishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania ili kujiridhisha kama wana sifa stahiki, uwezo na weledi katika kufanya kazi utunzi wa vitabu.

Awali, katika hotuba yake ya bajeti Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema, “Uchambuzi wa kina unafanyika kwa vitabu vyote vilivyochapishwa mwaka 2016/17 ili kubaini endapo kuna dosari zilizobainika...”

Alisema mchakato wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za utumishi umekwishaanza kwa watumishi ambao vitabu walivyoidhinisha vimebainika kuwa na makosa.

“Napenda kulihakikishia Bunge lako tukufu kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika ili kukomesha tabia ya uzembe kwenye kazi muhimu za Taifa,” alisema.

Alisema baada ya uchambuzi wa vitabu vyote vilivyochapwa kukamilika, wizara itaamua hatua za kuchukua dhidi ya vile ambavyo vitabainika kuwa na dosari.

“Nawahakikishia wabunge kuwa wazembe wote waliokuwa sio makini katika hili kuangalia vitabu hivi tutawaadhibu. Nawahakikishia tutasafisha taasisi hii (Taasisi ya Elimu Tanzania - TIE),” alisema.

Alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17, wabunge walishika shilingi katika mshahara wake kutokana na makosa katika vitabu vya kujifunzia.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni kweli lazima mabadiliko yafanywe hata ktk magaziti mengi kiswahili ni kibovu including bbc swahili [ online]

    ReplyDelete

Top Post Ad