WAZIRI Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Amenunua Hisa Za Vodacom Zenye Thamani Ya Tsh Milioni 20

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa amenunua hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania PLC zenye thamani ya Tsh. milioni 10 pamoja na nyingine za Tsh. milioni 10 kwa ajili ya mke wake, Mary Majaliwa ili kuwahamisha watanzania kuwekeza katika uchumi unaokuwa kwa kasi.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo Ijumaa, Mei 5, mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari mbele ya wakuu wa Masoko ya Hisa na Dhamana; Soko la Hisa la Dar es Salaam, viongozi wa Baraza la Uwezeshaji na kampuni ya Vodacom katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amewasihi Watanzania walioko ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kununua hisa hizo ili waweze kuwa wamiliki wa kampuni kupitia hisa zao. “Hii ni fursa kwa Watanzania kumiliki kampuni. Ukinunua hisa, unashiriki kikamilifu kumiliki kampuni na pia unaboresha uchumi wako binafsi. Ninawasihi Watanzania wote tumieni fursa hii kununua hisa hizo kabla muda haujaisha ili kuboresha uchumi wetu,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alimhakikishia Waziri Mkuu kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kuimarisha teknolojia yake ili kuwaunganisha watanzania na kuwezesha kukuza uchumi binafsi. Vodacom Tanzania ilianza kuuza hisa za awali mwezi Machi mwaka huu na mwisho wa kuuza hisa hizo itakuwa ni Mei 11, 2017.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akielekezwa jinsi ya kujaza fomu  za kununua hisa  za Vodacom Tanzania PLC na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities,Gerase Kamugisha  (kushoto) wakati alipokuwa akinunua hisa zake na mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani)zenye thamani ya shilingi milioni 20 katika hafla fupi  iliyofanyika ofisini kwake  jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji,Bi.Beng’i Issa  na Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad