ACT Wazalendo Hawataki Mchezo..Wasitisha Rasmi Uenyekiti wa Anna Mghwira

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chama cha ACT Wazalendo  kimesitisha rasmi uenyekiti wa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho tangu kuanzishwa kwake, Anna Mghwira, baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuazia tare ya leo Juni 7.

Uamuzi huo umefanywa na kikao cha Kamati ya Uongozi ya chama hicho ambacho pia kimemteua Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo, Oganaizesheni na Uanachama kuwa Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika mwezi Machi mwakani.

Akitangaza uamuzi huo kwa wanahabari leo, Kaimu Kiongozi wa chama hicho, Samson Mwigamba amesema sababu kuu ya kusitisha uenyekiti wa Anna Mghwira, ni ili kumpa nafasi ya kutekeleza majukumu yake mapya aliyopewa na Rais wa Tanzania, pamoja na kumfanya asiwe na mgongano wa kimaslahi ya kichama wakati akitekeleza majumu yake kama kiongozi.

Sisi kama ACT hatupingi uamuzi wa mamlaka ya Rais, isipokuwa kamati ya uongozi imeona ni busara kumpa nafasi Anna Mghwira kutumikia nafasi moja kama kiongozi, lakini ataendelea kuwa mwanachama wa ACT Wazalendo. Kabla ya kutangaza uamuzi huo tayari tumewasiliana naye na tumekubaliana hivyo. Tunamtakia kila la heri katika majukumu yake mapya,” amesema Ado Shaibu ambaye ni Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa umma.

Pamoja na hayo Mwigamba amempongeza  Rais kwa kuvunja miiko ya siasa za Tanzania kwa kumpatia mpinzani nafasi hiyo ndani ya serikali yake.  na kuongeza kuwa kama chama hawana tatizo kwa kiongozi huyo kukabidhiwa ilani ya CCM kwa sababu anakwenda kutumikia serikali kuu na Taifa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad