Baada ya Kimya Kirefu..Makonda Aibuka na Haya Makubwa Kuhusu Jeshi la Polisi...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema jeshi la Polisi katika Mkoa huo linatakiwa kuwa la mfano wa kuigwa katika kukabiliana na kila wimbi la uhalifu, ili wananchi waishi kwa amani kutokana na umuhimu wa biashara.

Makonda ameyasema hayo  wakati wa kupeleka magari 26 ya polisi kwenye ukarabati katika gereji iliyoko maeneo ya Utalii mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya matengenzo pamoja na ufungaji wa Kamera katika magari hayo alipokuwa anazungumza na jeshi la polisi leo Osterbay jijini Dar es Salaam.

Amesema katika kukabiliana na rushwa na jeshi hilo, watafunga kamera katika kila kituo ndani ya jiji la Dar es Salaam, ambapo OCD , kanda maalumu, pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi wataweza kuona kile ambacho kinafanyika.

Makonda amesema jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam linatakiwa kuwa la kisasa zaidi katika kukabiliana na uhalifu wa kila namna ikiwa ni pamoja na kuwa na vifaa vya kisasa.

Amesema katika maboresho hayo wataweka Kompyuta kila kituo ili kuachana na kuandika maelezo katika karatasi na mtu yeyote, baada ya kuwekwa kompyuta hizo asikubali kuandikiwa maelezo katika karatasi.

Aidha amesema kuna baiskeli ziko njiani ambazo zitagawiwa kwa polisi ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na uhalifu katika mazingira ambayo kifaa hicho kinaweza kupita.

Nae Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amesema Jeshi la Polisi kanda maalumu inakabiliwa na changamoto ya magari pamoja na mafuta na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi katika kukabiliana na wahalifu wa kila namna .

Amesema kuwa kutokana maboresho hayo yataweza kubadilisha hata takwimu zilizo katika kipindi hiki zisirudie kutokana na maboresho hayo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad