Ewura Yapandisha Bei ya Mafuta Kuanzia Leo Jun 17

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Nchini (EWURA) imetangaza bei mpya elekezi za mafuta zitakazoanza kutumika maeneo yote nchini kuanzia leo Juni 7, 2017.

Katika bei hizo mpya zilizotolewa jana na Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa EWURA, Titus Kaguo alisema kuwa kunaongezeko la bei katika mafuta ya petroli na dizeli huku mafuta ya taa yakishuka bei.

Kaguo alisema kuwa, ongezeko hilo la bei linatokana na sababu ya mabadiliko ya bei ya mafuta katika soko la dunia sambamba na kuimarika kwa thamani ya dola ya Marekani dhidi ya shilingi ya Tanzania.

Kwa upande wa mafuta ya dizeli yameongezeka Tsh 43 kwa lita huku mafuta ya petroli yakiongezeka Tsh 25 katika kila lita moja.

Aidha, afisa huyo alisema kuwa, bei hizo mpya haziwahusu wateja kutoka mkoa wa Tanga ambao wao wataendelea kutumia bei za mwezi uliopita kutokana na mkoa huo kuwa na bandari inayotumika kushushia na miundombinu ya kuhifadhi mafuta kiasi cha kuwa na akiba kubwa ya mafuta yaliyoingia nchini mwezi uliopita.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad