Fahamu – Vyakula Sita Asivyotakiwa Kula Mwanaume Riajali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chakula ni kitu muhimu kwenye maisha yetu, ila kunavyakula sita ambavyo mwanaume hastahiki ama haruhusiwi kula.

1. Punguza kula vyakula feki kuzuia kupoteza nywele


Vyakula feki (junk foods) ni hivyo vinapatikana kwenye fast foods na takeaway centers nyingi hasa mijini kadharika vyakula vile vyote vya kwenye maboksi.Vyakula hivi feki vina kiasi kingi mno cha lehemu (cholesterol) na lehemu hii hupelekea kile huitwa kwa kitaalamu kama ‘pregnenolone’ na kupelekea kiasi kikubwa cha ‘dihydrotestosterone’ (DHT) na hatimaye kupotea kwa nywele kichwani a.k.a upara.

2. Punguza kunywa pombe au acha kabisa kuzuia kuota matiti

Wanaume wengi wanaokunywa bia kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na tatizo la kuota matiti kama wamama tatizo lijulikanalo kwa kitaalamu kama ‘gynecomastia’.



Kwenye bia au pombe kuna kitu kama homoni ya oestrogen.Mara nyingi hakuna lishe ya moja kwa moja na hivyo hukufanya ujisikie njaa au hata kuongzeka kwa njaa zaidi na ndiyo sababu unaambiwa kama huna uhakika utakula wapi ni bora usinywe pombe ili kulinda afya yako.

3. Acha kutumia mafuta ya mboga mboga kuepuka saratani ya tezi dume

Mafuta yatokanayo na mboga mboga au mimea yamekuwa yakipigiwa debe kwa miaka mingi na watu wanaojihusisha na lishe na wale wenye hasira sana na mafuta yatokanayo na wanyama. Hata hivyo leo nakujulisha mafuta hayo si salama sana kutumika na mwanaume kila siku. Hili limekuja hasa kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ya moyo na lehemu na watu wakahimizwa kutumia mafuta ya namna hiyo.

Lakini mafuta haya ya mboga mboga ndiyo kitu kibovu kabisa unatakiwa kukiepuka ili usipatwe na saratani ya tezi dume. Linapokuja suala la kujilinda saratani ya tezi dume basi mafuta yenye omega 3 ndiyo suluhisho la kudumu na siyo omega 6 kama ilivyo kwenye vyakula vingi vya kwenye makopo, mafuta ya alizeti, maharage ya soya, mafuta ya canola na mafuta ya corn na mengine yote yenye omega 6.

4. Popcorn/Bisi


Popcorn au bisi ni chakula kingine mwanaume hatakiwi kula, hupikwa kwa kutumia mafuta yasiyo na afya, sodiamu nyingi na ni chanzo cha baadhi ya kansa. Kuna kitu kinaitwa ‘Diacetyl’ kinachopatikana kwenye popcorn ambacho kinahusika na kusababisha kansa na kuna kingine kiitwacho ‘Perfluorochemicals’ ambacho huathiri tezi ya thyroid na ugonjwa wakati huo huo husababisha ugonjwa wa kupungukiwa umakini ujulikanao kwa kiingereza kama ‘Attention-deficit/hyperactivity disorder (ADHD)‘.

5. Mkate mweupe

Mkate mweupe una wanga mwingi zaidi usio na faida. Kwenye hatua za kutengeneza mkate mweupe vitamini zote za kundi B hupotea, hupotea pia nyuzinyuzi (fiber). Siyo hivyo tu mkate mweupe umesemekana kuwa ni sababu ya ugonjwa wa kisukari na kuongeza uzito zaidi mwilini wakati huo huo ukisababisha tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.


Kula mkate ambao ngano yake haikukobolewa (brown bread), kula ugali wa dona na chai unaweza kutumia tangawizi au mdalasini badala ya majani ya chai.

6. Chumvi ya mezani



Chumvi ya mezani ile ya unga nyeupe haifai kwa mwanaume. Kila mmoja amesikia chumvi hii husababisha shinikizo la juu la damu na pamoja na hayo bado sehemu kubwa ya watu wanatumia chumvi hii.
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi kwa afya ya mwanaume.

Chanzo Dk Fadhili Paulo
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad