Mkude: Kwa dau hili nipo tayari kujiunga na Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


UNAWEZA ukashituka kidogo ila habari ndiyo hivyo anaweza kusaini Yanga kwa milioni 70 tu, Mkude ambaye mara kadhaa amewahi kuhusishwa kuwaniwa na Yanga ameamua kuweka wazi kuwa atatua ndani ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya kukitumikia msimu ujao kwa kutoa sharti moja kubwa ambalo ni klabu hiyo kumpatia shilingi milioni 70.

Mkude kwa sasa yuko huru kujiunga na timu yoyote baada ya mkataba wake na Simba kudaiwa kumalizika hivi karibuni, ikiwa ni mwisho wa mkataba wake wa shilingi milioni 60 aliosaini kuitumikia Simba miaka miwili iliyopita.

Akizungumza kiungo huyo, amesema atakuwa tayari kusaini mkataba na klabu ya Yanga kwa dau la kuanzia milioni 70 kwenda juu kutokana na kiwango alichonacho kwa sasa. Simba wamempa ofa ya milioni 40-50 ila yeye amekataa kwa kigezo kwamba mkataba unaoisha walimpa milioni 60 kwa sasa lazima dau lipande.

“Kwa upande wangu nipo tayari kutua Yanga kwa dau la kuanzia milioni 70 na kuendelea hadi shilingi milioni 150 na siwezi kusaini chini ya hapo, nipo tayari kutua katika timu yoyote kwa kiasi ambacho tutakubaliana kwa kuwa kiwango changu kipo vizuri.

Nahodha huyo wa Simba amesema lolote linaweza kutokea kuanzia sasa: “Tusubiri kila kitu kitakuwa wazi muda si mrefu na wadau watajua nitasaini wapi kwa ajili ya msimu ujao, wasiwe na hofu.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad