Mtanzania Atupwa Jela Uingereza Kwa Kutupia Picha za Marehemu Facebook

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanaume mmoja anayedaiwa kuwa ni Mtanzania amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela nchini Uingereza kwa kosa la kurusha katika ukurasa wake wa Facebook, picha za mtu aliyefariki dunia kutokana na moto uliounguza jengo la ghorofa la Mnara wa Grenfell lililopo nchini humo.

Pia, mtu huyo ametakiwa kulipa faini ya Sh579,880 kwa mwathirika wa tukio hilo.

 Mtanzania huyo, Omega Mwaikambo (43) alituma video na picha za mwili wa marehemu uliokuwa kwenye begi  na baadaye picha nyingine tano zikionyesha uso wa  marehemu huyo.

Gazeti la mtandaoni la The Telegraph limeandika kuwa Mwaikambo amekiri makosa ya kutuma mara mbili picha zisizopendeza kwa umma katika mitandao ya kijamii mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Westminster jana.

Mwaikambo ambaye anaishi hatua chache kutoka lilipo jengo la Grenfell akifanya shughuli za upishi, alishuhudia jinsi jengo hilo lilivyoungua moto usiku na alikuwa ni miongoni mwa wapishi waliowapikia chai wafanyakazi wa zimamoto walipokuwa wakizima moto huo.

“Lakini juzi Jumatano asubuhi alipoangalia miili hiyo nje ya nyumba yake alichukua picha kwa kutumia simu yake aina ya iPad na kuzipakia kwenye mtandao wake wa Facebook,” liliandika gazeti hilo.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Tom Little amesema; “Anaishi karibu zaidi na mnara wa Grenfell, kama ambavyo mahakama inajua janga hilo lilitokea Juni 14.”

Akitoa hukumu, Jaji wa mahakama hiyo, Tanweer Ikram amesema; “Dunia nzima imeshtushwa na yaliyotokea hapa kutokana na janga la moto, ni hali ya kutisha isiyostahimilika, wafu ni lazima waheshimiwe.”

Ameongeza; “Ulichokifanya kupakia hizo picha kwenye Facebook ni dhahiri kuwa hujaonyesha heshima kwa waathirika wa tukio hilo, kuonyesha uso wake  hadharani ni kosa kubwa na halielezeki.”

Mpaka sasa watu zaidi ya 17 wanadaiwa kufariki dunia kutokana na moto uliounguza jengo hilo refu na maarufu Magharibi mwa Uingereza.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad