Serikali Yaomba Radhi Walemavu Kupigwa Dar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali imewaomba radhi walemavu na Watanzania wote kutokana na nguvu kubwa iliyotumika kwa walemavu waendesha bajaji wa Jiji la Dar es Salaam waliokuwa wakitaka kwenda kumuona Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ameomba radhi leo (Jumanne) na kukiri kuwa pamoja na walemavu hao kuwa na makossa, lakini nguvu ya polisi ilipitiliza na akasema wameshawasilina na mkoa husika kupitia ustawi wa jamii.

Waziri alikuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu, Stella Ikupa ambaye alitaka kujua namna gani Serikali inavyoweza kuliona jambo hilo lililosababisha walemavu kupigwa, kuburuzwa chini na kudhalilishwa kwa kiasi kikubwa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Si kwa mara ya kwanza seriksli kutumia vyombo vya dola ambavyo ni vya wananchi kushambulia. Elimu ya ukoloni, elimu ya unyampala, elimu ya zsmani. Ya woga, nguvu, uonezi badala ya kutoa elimu safi na kuweka mahusiano safi na wananchi mnatumia vitisho, mabavu, dhuruma, na mspigo kwa hata wansnchi wanaotafuta haki zao. Mmefanya hivi kwa miaka mingi, kwa wapinzani na bado mnaendelea. Juzi serikali ilisema ruksa kukosoa, leo mnawabana wapinzani hata kufanya kazi za maendrleo. Kutumia polisi ambao kazi zao ni kutuliza fujo, kulinda amani, kumlinda kila mtanzania na mali zao. Leo mnatumia polisi kichama kuwapiga, kuwapeleka mahakamsni, na watu wametekwa na vyombo vya usalama kupitia uongozi wa CCM. Mtu yeyote wa CCM ambaye haoni uonevu huu kwa raia wasio na hatia na wanaunga mkono nawashangaa jinsi wanavyotumia pesa zao za kodi kwa kutokutaka amani, uhuru, na majadiliano bila mvutano ambayo ni muhimu kwa Taifa hili. Ukichochea moto usishangae ukikulipukia.kumfanya mtu mzima asitumie akili yake kufikiri na kumlazimisha aone mazuri yako ingawa si mazuri ndiyo tunayokabiliana nayo baada ya kufungwa midomo zaidi ya miaka kumi.mtu kimyamazisha, kumwonea kila siku hujui ndani mwake kunawaza nini.na usishangae likiwska sababu umelitengeneza. Wengi wakaao kimya huwa waoga, au wamehusika kwa namna hii au nyingine au uwezo wa kufikiri mdogo. Lakini kwa polisi kupiga vilema kama mbwa, kama duni, bila kumwona huyu ni binadamu hapa tunaingia Iraq na si Tanzania.ni aibu kwa taifa letu kuona haya mambo ambayo wajerumani waliwapiga na kuwadharalisha babu zetu hadharani kama wanyama. Na waingereza walifanya hivi pia. Lakini kwa miaka ya sasa kumyanyasa binadamu kama kondoo bila kujisikia vibaya kwa unalolifanya. Hii sina neno la kufananisha.Najua watu wa vijijini wengi hawana mwamko hasa vijiji vilivyosahauliwa kwa muda mwingi. Na Ccm inakwrnda kuwaambia upinzani wabaya, hii chuki itaingiza nchi yetu njia panda. Waziri unataka ushirikiano na wananchi utaupataje kama unatumia polisi haohao kupiga, kukamata.hutapata ushirikiano hata. Hutapata ukweli hata. Tawafunga watu midomo ndiyo, lakini hutatatua tatizo lolote. Tunamhitaji waziri mkomavu, shupavu, mwenye maadili, hekima, uvumilivu ili aweze kujishusha kuwa sawa na raia wa kawaida ili aaminike na watu wajisikie huru kuongea na kutoa na kuchangia mawazo bila kunyanyaswa. Si hivi. Sikubaliani na mambo mengi sana viongozi na vyombo vya dola mnavyonyanyasa na papara mnazozifanta. Hawa vilema na kila mliyemwonea anakuwa adui yenu na mnawatengeneza wawe adui.inasikitisha sana.hekima, akili ,elimu, shari, nguvu na ibada. Ukivifanya hivi vyote hutakuwa na papara. Uovu umeshaufanya hata ukiomba msamaha watu wanamakovu.

    ReplyDelete

Top Post Ad