Mkurugenzi wa Zamani FBI Amlipua Trump

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Donald Trump
Washington, Marekani. Aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), James Comey ameishtumu Ikulu ya Marekani kwa kumharibia jina na kusema uongo kuhusu shirika hilo.

Comey ambaye aliyefutwa kazi ghafla na Rais Donald Trump alisema hayo jana Alhamisi, baada ya kuanza kutoa ushahidi mbele ya maseneta nchini Marekani kuhusu tuhuma kwamba Urusi iliingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka uliopita.

Mkuu huyo wa zamani wa FBI amewaambia maseneta waliomhoji kuwa alikuwa na mazungmzo ya siri na Rais Trump. Aidha, ameshtumu matamshi ya Ikulu ya Marekani kuwa FBI ilikosa imani naye.

Trump alimfuta kazi Comey Mei 9, mwaka huu baada ya FBI kutangaza kuchunguza madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani, madai ambayo Urusi imekanusha.

Comey amesema, Trump alimwambia asitishe mchakato wa FBI kumchunguza Michael Flynn, aliyekuwa mshauri wake wa masuala ya usalama wa Taifa kwa madai kuwa alikuwa na mawasiliano ya karibu na maofisa wa Urusi kipindi cha uchaguzi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad