Wabunge Wajazana Mgahawani Bungeni Kushuhudia Ripoti ya Pili ya Mchanga wa Madini Kwenye Luninga..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bungeni

Wakati kipindi cha maswali na majibu kikiendelea bungeni leo Jumatatu, baadhi ya wawakilishi wametoka ukumbini na kwenda kantini ya Bunge kufuatilia ripoti ya pili ya usafirishaji wa mchanga wa dhahabu inayorushwa mubashara kupitia vituo vya televisheni kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baadhi wa wabunge wakinywa chai huku wengine wakijiburudisha kwa vinywaji baridi wamekuwa kwenye makundi matatu kulingana na idadi ya runinga zilizopo katika kantini hiyo.

Ilipotajwa hoja ya udanganyifu katika taarifa inayotolewa kisha Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wake, Kassim Majaliwa kuonekana kwenye kioo cha televisheni wakitazamana, wengi wameguna ishara kwamba hoja hiyo ni nzito.

 Hata yaliposomwa makosa ya jinai yanayoambatana na usafirishaji huo, miguno mingine imesikika.

 Ukwepaji kodi, udanganyifu na makosa mengine yaliyobainishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo ya pili, yamewagusa wabunge wengi wanaofuatilia.

 Bila kujua kama wanaambizana au ni shauku ya kila mmoja kusikia kinachowasilishwa na kamati hiyo, idadi yao imekuwa ikiendelea kuongezeka kantini.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad