Wakamatwa na Dawa za Kulevya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la Polisi Mwanza linawashikilia watu wanne baada ya kuwakuta na dawa za kulevya aina ya Mirungi mafungu 57 yenye ukubwa wa kilogramu 56.75 ambayo yalikuwa yamewekwa kwenye mabegi na magunia.

Watuhumiwa wanne waliokutwa dawa za kulevya aina ya mirungi Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa polisi waliwakamata watuhumiwa hao leo majira ya saa kumi na moja alfajiri katika mtaa wa Mbugani 'A' Kata ya Mbugani wilayani Nyamagana.

"Askari wakiwa kwenye doria na misako walifanikiwa kuwakamata watu wa nne waliofahamika kwa majina ya Thomas Zacharia (25), mkazi wa mtaa wa Unguja Mwanza, Ally Athumani (35) mkazi wa Kahama Shinyanga, Nyamurya Elia (35) mkazi wa mtaa wa Unguja Mwanza, na Stanslaus Mapinduzi Elias (41) mkazi wa Tarime, wakiwa na dawa za kulevya aina ya mirungi mafungu 57, yenye kiasi cha kilogramu 56.75, yakiwa yamemewekwa kwenye mabegi na magunia, kitendo ambacho ni kosa la jinai" ilisema taarifa ya Msangi

Kufuatia sakata hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa Mwanza hususani vijana akiwataka kuacha kujihusisha na biashara za madawa kwani ni kosa kisheria.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad