EXCLUSIVE: Fahamu Mambo 8 kuhusu Train za umeme zinazoletwa Tanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais JPM April 12, 2017 alizindua ujenzi wa reli ya kisasa ‘standard gauge’ kutoka DSM hadi Mwanza ambayo itakamilika Oct 2019 jambo lililozua gumzo kwa baadhi ya Wananchi wakiwa na wasiwasi kuhusu train hizo kutokana na tatizo la umeme.

Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Mhandisi wa Miundombinu ya Reli ambaye pia ni Mkuu wa Mradi huu Maizo Mgeni kutoka Kampuni inayojihusisha na ujenzi wa reli Tanzania RAHCO na kuelezeea mambo makubwa manane yanayohusiana na Standard Gauge.

Mambo manane hayo ni:

1: Treni itakuwa inasimama kwenye vituo sita kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo itasimama Pugu, Soga, ruvu, Stesheni ya Ngerengere na mwisho Treni itasimama Morogoro.

2: Kutokana na Treni kutumia umeme Serikali imejipanga kutoa umeme wa uhakika kwa 100% na wananchi wasiwe na shaka yoyote kwani umeme wa Treni hujengewa nyaya zake maalum zinazotofautiana na nyaya za umeme wa kawaida.

3: Treni hii itakuwa na uwezo wa kusafirisha wagonjwa mahututi kwani ni za kisasa na zina mwendo wa haraka ambapo itatumia saa moja na nusu kutoka Morogoro hadi Dar es Salaam.

4: Umeme utatumia vyanzo vyenye nguvu kutoa umeme wa Treni kama vyanzo vya maji na makaa ya mawe.


5: Kwa tathmini ya sasa nauli ya Treni hizi haitokuwa sawa na Treni za mita kwani ni Treni zinazotumia teknolojia kubwa na za kisasa, hivyo nauli itakuwa juu zaidi ya Treni za kawaida.

6: Treni haitosimama kama umeme kutoka Tanesco ukikatika ghafla.

7: Kiwango cha nauli kwa wanafunzi bado kinafanyiwa kazi.

8: Kwa sasa watu binafsi hawataruhusiwa kuwa na Treni binafsi kwani Shirika la Reli ndilo litakuwa msimamizi mkuu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad