WATUMISHA Wavivu wa Serikali Kukiona Cha Moto...Mishahara Kufyekwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BUNGE limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, na sasa sheria imetamka kuwa ofi sa wa umma aliyesababishia serikali au taasisi ya umma kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa makusudi au kwa uzembe, atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kukatwa mshahara wa miezi sita.

Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amesema mabadiliko ya Sheria ya Bajeti na yale ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yaliyopitishwa jana bungeni, hayakusudii kupoka kwa namna yoyote ile mamlaka ya kisheria ya Bunge.

Kifungu cha 65(2) cha Sheria ya Bajeti kinaweka masharti kuwa iwapo itathibitika kuwa ofisa wa umma kwa makusudi au kutokana na uzembe, alisababisha serikali au taasisi ya umma kushindwa kutekeleza majukumu yake chini ya sheria hiyo, atatenda kosa la kinidhamu.

Masaju alisema atawajibishwa binafsi kwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu au kushtakiwa kwa kosa la jinai kulingana na aina ya madhara yatokanayo na kushindwa majukumu hayo.

Kuhusu uhamisho wa fedha, alisema baada ya mabadiliko hayo hivi sasa uwasilishaji wa taarifa za uhamisho wa fedha na uwasilishaji wa taarifa za serikali na taarifa za mapato na matumizi, zitawasilishwa kila baada ya miezi sita kwa maana ya nusu mwaka, badala ya miezi mitatu kwa maana ya robo mwaka kama ilivyokuwa awali.

Akihitimisha hoja yake aliyoiwasilisha bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2017, ambayo ndani yake ililenga kufanya mabadiliko katika Sheria ya Bajeti na mabadiliko ya sheria ya ofisi yake, Masaju alisema kimsingi muswada huo sio wa kubadilisha kanuni za haki na madaraka ya Bunge wala madaraka ya Kamati ya Bajeti kama baadhi ya wabunge wanavyodhani
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Naona hizo diploma zenu mlizotunukiwa kama waandishi wa habari zina"WALAKINI"

    ReplyDelete

Top Post Ad