Mgogoro wa CUF Bado Ngoma Nzito..Lipumba Atangaza Kuwafuta Uanachama Wabunge 8 CUF

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limewavua uanachama wabunge wanane wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu, yakiwemo kukisaliti chama hicho.
Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema, baraza pia limewavua uanachama madiwani wawili wa viti maalumu mkoani Dar es Salaam, kwa makosa kama hayo.

Profesa Lipumba ametangaza uamuzi huo leo Jumatatu, Julai 24 wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika makao makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam.

“Leo asubuhi tumewasilisha nyaraka  za hatua hizi kwa Spika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa hatua zaidi,” amesema Profesa Lipumba.

Amesema wabunge hao wanane ni kati ya 10 walioitwa hivi karibuni na Kamati ya Maadili na Nidhamu kwa mahojiano wakitakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili za kukihujumu chama hicho kwa maelezo kuwa walitaka kushirikiana na Chadema kumwondoa yeye madarakani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad