‘Tanzania Haina Uwezo Kudhibiti Uhalifu’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

By Aurea Simtowe
Tanzania haina uwezo wa kudhibiti uhalifu wa kimtandao kutokana na mitandao inayotumika kumilikiwa na watu wa Magharibi.

Kauli hiyo imetolewa jana katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa Serikali kutoka Tanzania na China na wawakilishi wa vyombo vya habari jana.

Mkutano huo ulikuwa ukidhibiti matumizi mabaya ya mtandao yanayoweza kuleta madhara katika vyombo vya habari.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amesema sheria ya udukuzi wa kimtandao inayotumika nchini haina uwezo wa kuwawajibisha watu wanaotumia vibaya mtandao kutokana na tofauti za tamaduni.

“Sasa tuna watu wanaodhibiti wahalifu wa kimtandao, lakini wanapata wakati mgumu kuthibitisha ushahidi kupitia mitandao ya kijamii kwa sababu mingi inatoka Marekani na kusimamiwa na sheria za nchi hiyo,” amesema Ngonyani.

Balozi wa China nchini, Lu Youqing amesema Tanzania ni moja kati ya nchi barani Afrika ambayo matumizi ya kimtandao yanakua kwa kasi, hivyo ni lazima kuwe na udhibiti wa watumiaji wabaya.

“Kupitia takwimu za TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania) zinaonyesha kuna ongezeko la mara 13.7 kwa watumiaji wa simu ndani ya miaka 10 kutoka milioni 2.9 mwaka 2005 hadi kufikia watu milioni 39.8 mwaka 2015, huku watumiaji wa tovuti wakifikia milioni 17.26 mwaka 2015 kutoka milioni 1.01 mwaka 2005,” amesema  Balozi Youqing.

Mwananchi
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad