Ukweli Mchungu....Wanawake 556 Kati 1000 Hufariki kwa Uzazi..Sababu Hizi Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Aga Khan, Eunice Pallangyo amefanya utafiti katika wilaya ya Ilala na kubaini kwamba vifo vya akinamama wilayani humo husababishwa na mambo mbalimbali, ikiwamo kutokuwepo huduma ya uangalizi baada ya kujifungua.

Akizungumzia utafiti huo leo , Dk Pallangyo amesema amebaini hayo, baada ya kutembelea vituo vya afya na hospitali 27 za wilaya hiyo na kuwa  huduma hiyo haitolewi ipasavyo licha ya mwongozo wa wizara ya afya kuagiza hivyo.

Dk Pallangyo amesema takwimu za wizara zinaonyesha kwamba wanawake 556 kati 1000 hufariki kwa sababu ya matatizo wakati wa kujifungua
“Wanawake huondoka hospitali saa chache baada ya kujifungua bila kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara,” alisema Pallangyo
Mbali na hilo Pallangyo amedai mwongozo wa wizara unataka mwanamke aliyejifungua kuchunguzwa mara kwa mara katika kipindi cha siku 42 za mwanzo. Amesema watoa huduma aliozungumza nao wamesema hawatoi huduma hiyo kwa sababu ya upungufu wa wafanyakazi na ufinyu wa nafasi katika vituo vya afya.

Hata wazazi waliohojiwa wengi walionyesha kutokuwa na elimu sahihi ya masuala ya uzazi. "Kwa hiyo serikali imeweka miongozo ambayo watendaji wake hawaitekelezi kwa sababu ya changamoto zilizopo."Alidai Pallangyo
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad