Jerry Muro Ageukia Siasa...Amchana Chana Vibaya Rais wa TLS Tundu Lissu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tundu Lissu, TUNDUNI
Na Jerry C. Muro

Nianze kwa Kutoa pole kwa jumuiya nzima ya wanasheria nchini, pole yangu sio ya tukio la IMMA advocates, Bali pole yangu ni ya kuchagua Rais wa TLS Chama Chenu 'MAHIRI' cha wanasheria Tanganyika - TLS Ndugu Tundu Lissu ambae AMEDHIHIRISHA kuwa ameanza Rasmi Safari ya Kuizika TLS, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari kuhusiana na Tukio la IMMA advocates.
Nianze kwa kuweka msingi wa HOJA yangu kuwa sifurahishwi na kilichotokea kwenye IMMA advocates, ila pia SIFURAHISHWI zaidi na "AKILI NDOGO" za Rais wenu katika hatua za AWALI za kushughulikia suala hili.

Mimi ni Profesional communicator kama mwandishi wa Habari, na Nyinyi wanasheria ni Profesional kwenye Sheria, ukisoma na Kusikiliza kwa umakini TAARIFA ya Mhe Rais wa TLS utagundua makosa makubwa sana ya KIUFUNDI ambayo yanaifanya taarifa nzima kuwa kama taarifa ya Mfalme "****" na kwa sisi MAFUNDI wa taarifa tunasema taarifa ikikosewa katika UANDAAJI na UWASILISHWAJI inakuwa imekosa MASHIKO, na hivyo taarifa nzima kuwa BATILI.

KWANINI BATILI
1. Taarifa iliyowasilishwa na Rais wa TLS tayari kwa kiasi kikubwaa ilishatolewa na Chama cha wananchi CUF #teammaalim, ukisoma taarifa ya cuf ambayo ilitoka siku moja kabla ya hii ya Rais utaona nachosema, ila hii ya Rais imewaka mbwembwe ya Vifungu Vifungu vingi vya SHERIA tu, ila taarifa zote zimeonyesha kuwa IMMA advocate ni WABIA katika kazi mana cuf inatetewa na IMMA advocate na Rais Lissu anatetewa na IMMA advocate hivyo wote WANAOMBELEZA DHORUBA YA MMBIA WAO., japo TLS ni Chama na Lissu ni Rais, na ni mteja wa IMMA katika hoja hii ya kwanza nimalizie kwa kusema tu Hoi taarifa ni BATILI kwa kuwa Imekuwa taarifa ya KISIASA na Imetolewa na wanasiasa wa vyama viwili tofauti, japo Mmoja ni Rais wa TLS, hapa utaona sasa Hatari ya kuwa na Rais wa TLS ambae ni mwanasiasa.

2. Taarifa ni BATILI kwa kuwa imeanza kwanza kwa KUHUKUMU kuwa Ofisi za IMMA advocate zimepigwa BOMU na POLISI, japo hizi ni taarifa za AWALI lakini kwa maoni yangu TAARIFA haikupaswa kujielekeza kwenye kazi za mamlaka nyingine, mana kama mmeshajua waliolipua ni POLISI basi hamkuitaji kutoa taarifa Bali kufuata SHERIA kuwashtaki POLISI.
Katika hoja hii MWENDELEZO wake inasema wanavitaka vyombo husika wakiwemo "WATUHUMIWA" Polisi kufanya uchunguzi, mbele zaidi tena wanataka kukutana na "MTUHUMIWA" boss wao IGP, hivi hii ni SAWA WANASHERIA, mnataka kukutana kufanya nini tena na IGP au mkurugenzi wa usalama wa taifa ambae majuzi juzi hapa wakati wa Sakata la Bombadier Rais "WENU "alishema kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa" ANAMFUATILIA FUATILIA "sasa iweje Leo aombe mwenyewe kukutana na" MTESI " wake, NDIO MANA NASEMA HAPA KUNA TATIZO YA HIKI CHAMA KUONGOZWA NA MWANASIASA, labda niwakumbushe tu hawa wanasiasa enzi ya Lowassa Walisema" mwizi" alipokwenda kwao wakamuita mfalme wa AMANI hawa ndio wana SIASA.

3. Taarifa ni BATILI, kwa sababu taarifa inataka WANASHERIA kugoma jumanne na jumatano, huu ni MGOMO ambao katika taarifa yao wanaomba ufanywe UCHUNGUZI, lakini pia kwenye taarifa yao wanaomba kuonana na kaimu Jaji Mkuu ambae mmekuja kusema tena hapo Chini ASUSIWE hamtaki kwenda kwenye mahakama anazoziongoza, JAMANI mnajua mnachofanya? Hii ni sawa na KUJITEKENYA MWENYEWE KISHA UKACHEKA MWENYEWE. nadhani Wasomi wana Sheria tukubaliane katika jambo moja MGOMO au KUONANA na "WATESI "wenu huwezi kushika mambo mawili kwa wakati Mmoja lazima MOJA litaponyoka.

4. Hii taarifa ni BATILI, kwa sababu imemtangaza MGOMO pasipo kusema ADUI ni Nani, hivi Hebu tuambieni mnagoma mkilenga KUMUUMIZA Nani? Kuwaumiza wateja wenu walioko MAGEREZANI au? Hivi nyinyi hii kazi ya UANASHERIA ni ya kujitolea katika kazi zenu zote? Hivi hakuna pesa mmechukua za wateja wenu ambazo mnapaswa kuzifanyia kazi, au TUSEME na nyinyi "WEZI" mnachukua hela za wateja wenu kisha mnagoma?
Hebu mtuambie Nani ADUI YENU basi.

MASWALI MAGUMU ZAIDI TLS.

1. Hivi Mbona walipouwawa *WANASHERIA* na *MAWAKILI* nguli nchini, tena waliowasomesha na kuwafundisha *HAMKUGOMA KUSHINIKIZA HAKI ITENDEKE KAMA HIVI LEO,* au mmesahau Vifo vya *"UTATA"* vya Mawakili Marehemu Kapinga, Marehemu Mvungi, Marehemu Mwaikusa? Kwa kuwa mnasahau ngoja tuwakumbushe tu *HAKUNA NAMNA*, Leo hao wazee wamekuwa *"LIABILITY"* kwenu halafu cuf, Lissu, acaccia zimekuwa *"ASSET"*kwenu?

2. Hivi tangu lini mmeanza kushirikiana press releases na vyama vya siasa mfano cuf?

3. Hivi TLS kimekuwa Chama cha Siasa, au kwakuwa Rais wenu ni mwanasiasa?

4. Mnawezaje kuitenganisha TLS na siasa?

5. Katika Sheria kuna neno linaitwa *"INNUENDO"*hivi mnajua maana ya hilo neno katika Sakata hili la IMMA advocate?

6. Hivi mnajua IMMA advocate ni kampuni "inayotajwa" KUCHOTA mabilioni ya fedha za EPA kupitia kampuni ya DEEP GREEN kiasi cha *BIlioni 8* zilichotwa, mnajua hilo? kama hamjui nendeni Brella kisha mkasome anuani za Kampuni ya *DEEP GREEN,* kisha mtangaze *MGOMO.*

7. Hivi mnajua huyu Rais wenu Lissu akiwa Bungeni mwaka 2012 Aliitaja kampuni ya IMMA advocate kuwa ilizitetea kampuni za TanGold na Deep green microfinances *KUCHOTA* pesa za EPA, halafu Leo HAWAHAWA imma advocate ndio wanaomtetea Lissu katika kesi zake?

Hivi mnajua maana ya vita ya *KIUCHUMI,* adui yako anaweza kutumia *MKEO, WATOTO* na hata Ndugu zako ili mradi *APATE USHINDI.*

Mwisho, Nawapenda sana *WANASHERIA,* mana najua mchango wao katika taifa la Tanzania, nawathamini sana Wanasheria wamaotanguliza *UZALENDO* kwa taifa Lao pamoja na changamoto tunazopitia kama taifa Changa, Nawapenda Wanasheria wanaosem *KWELI* kwa maslahi ya taifa Lao na Sio *MATUMBO* yao.

Sasa Sikilizeni, *AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO.LEO TUNDU, TUNDUNI.*

Wasalamu
*Jerry C. Muro*
*28/08 /2017*
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jerry Muro na dalili za kujipendekeza ili kupata nafasi ya kugombea ubunge kupitia chama tawala.

    ReplyDelete
  2. Muro katumwa na rafiki yake .rafiki yake nadhani mnamjua

    ReplyDelete
  3. Jerry. Asantr Sana kwa kubainisha haya ya Ukweli mtupi. Lisu Ni mchovhezi na hajitambui na hatambui anacho kisema na kukifanya. Anataka kugeuza TLS kuwa Ni segemu ya chama chake na kutaka kuhamasisha watu dhidi ya serekari tawala.
    Je ameweza kudikiria kwa akili ndiyo Tu kama ya kuku usumbufu ambao ungeathiri wadai haki zao.
    Leo ameweza kufungua kinywa chake kuhamasisha. Hapo watu wametunia Akili ba kumuona Ni mpuuzi.
    Huyu ataripoti Central na atashughulikiwa ipasavyo.
    MWWBYE TABIA HAACHI

    ReplyDelete
  4. Jerry yanga wanakuita ukahubiri siasa maana ushazoea kutukanwa

    ReplyDelete
  5. PENYE UKWELI UONGO UJITENGA.!!!!

    ReplyDelete
  6. Kwa rahisi huyo toka chadema, wajiandae na migomo kila uchao, tena sina shaka hata hilo bomu wamelitega wao wenyewe

    ReplyDelete
  7. Hongera Jerry kwa uliyoyaandika. Tukiwa ambiance "wasomi" wetu vibaya katikati TLS kuwa Bw. Tundu asingaliweza kutenganisha sasa na taabu mama wanasemaje similar ni wazee tumefiwa na wakati. Anayesema unatumiwa haijui misingi ya kuliko kwa TLS na jinsi ambavyo heshima yetu kama mawakili imemomonyoka. TUJISAHIHISHE HARAKA. Dr. Masumbuko Lamwai wakili namba 445.

    ReplyDelete
  8. KUMBE JERRY KICHWA HIVI????,AWALI NLIKUWA SIJUHI:BIG UP BABA UNAONA MBALI.HUYO RAIS NI MCHOCHEZI NAMBA MOJA KWA MASLAHI YA TUMBO LAKE...

    ReplyDelete

Top Post Ad