Kesi ya Kugushi Nyaraka ya Aveva na Kaburu Yazidi Kuwaweka Lumande

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kesi ya Kugushi Nyaraka ya  Aveva na Kaburu Yazidi Kuwaweka Lumande
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Agosti 16, 2017 imeahirisha kwa mara nyingine kesi ya kutakatisha fedha na kughushi nyaraka inayowakabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu hadi Agosti 30 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Victoria Nongwa baada ya Wakili wa upande wa mashitaka kueleza kuwa kwa vile nyaraka za kughushi maandiko zinahitaji utaalam kuzibaini, hivyo kitengo maalum cha kubaini maandishi kinaendelea kufanya uchunguzi ili kukamilisha upelezi huo ambapo aliomba kesi hiyo isogezwe mbele kwa siku 14 ili kukamilisha uchunguzi.

Hakimu Victoria Nongwa aliutaka upande wa mashtaka kukamilisha haraka upelezi wao ili kesi hiyo ianze kusikilizwa ambapo aliisogeza hadi Agosti 30 ili kuwapa nafasi kukamilisha upelelezi wao huku watuhumiwa wakirudishwa gerezani.

Aveva na Kaburu wanashtakiwa na TAKUKURU wakikabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba na kutakatisha dola za Marekani 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad