Kipusa ya Ali Kiba ni Moto wa Kuotea Mbali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kipusa ya Ali Kiba ni Moto wa Kuotea Mbali
BAADA ya ukimya wa muda mrefu wa kutoachia ngoma mpya, staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ aliwaweka kwenye ‘kimuhemuhe’ mashabiki wake kwa kuonesha dalili za kuachia wimbo mpya ambao ulishakuwa maarufu kabla hata haujatoka.

Mkali huyu ambaye alikimbiza na wimbo wa Aje alioutoa mwaka jana, kwa kipindi chote hicho alikaa kimya na sasa ‘ameuvuruga’ ulimwengu wa burudani kwa ‘kubipu’ na posti zinazoashiria wimbo wake mpya uitwao Kipusa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye mashabiki zaidi ya milioni mbili, Kiba alianza kutupia picha zilizoandikwa Kipusa na kuwafanya mashabiki wake wapagawe kwa kumtaka autoe wimbo huo haraka iwezekanavyo.

“I cant wait Kiba, achia bwana hiyo Kipusa iwakimbize wote wenye nyimbo mbovumbovu mjini,” aliandika mmoja wa wafuasi wa Instagram. KING NI KING Kiba ana historia ya kutoa wimbo au nyimbo kadhaa na zikakaa kwenye soko kwa muda mrefu tofauti hata na yule msanii anayejidai kuwa ni mpinzani wake wa jadi ambaye kila siku anatoa nyimbo lakini hazikai muda mrefu kwenye soko, zinaotea.

USHAHIDI NI HUU
Kabla ya Kiba hajatoa Chekecha Cheketua mwaka 2015, alikuwa kimya kwa muda mrefu lakini mashabiki wake waliendelea kusikiliza ngoma za kitambo kama Cindelera na Kidela. Alipoibuka mwaka huo, kila mmoja alikubaliana na ujio wake wa  Chekecha Cheketua kabla hajachagiza na Aje kisha Mwana. Hapo ndipo kila mtu alimjua Kiba ni nani. Kila mtaa, kila nyumba watu walisikika wakicheza nyimbo hizo za Kiba ambapo alidhihirisha ule usemi wake wa ‘nimepangusa kiti changu kilichokuwa na vumbi kisha nakikalia tena’.

UTOFAUTI WA KIBA
Tofauti na wasanii wengine, Kiba ni mwanamuziki. Namaanisha msingi wake umejengeka katika muziki. Anajua kuimba na vyombo, tofauti na wasanii wengi wa Bongo Fleva ambao ukiwaambia waimbe kwa vyombo, wataingia mitini.

HADI SASA HAKUPOA
Baada ya kuachia ngoma hizo, Kiba alikaa tena kimya hadi jana alipoaamua kuachia ngoma yake ya Kipusa (video na audio) na tayari imekuwa gumzo kila kona ya jiji.

SHOO KIBAO NJE YA NCHI
Kuonesha kwamba Kiba yupo vizuri, kwa wakati wote huo amekuwa akifanya shoo nyingi nje ya nchi.

AMEPIGA SHOO NEW YORK, MAREKANI
Huyo ndiye Kiba ambaye hata mwishoni mwa wiki iliyopita, aliandika historia kwa kufanya shoo matata sana pande za Marekani.

KOLABO KALI
Moja kati ya sifa nyingine kubwa ambayo Kiba anayo, amefanya kolabo nyingi sana ambazo kimsingi, hazijawaacha salama wenye nyimbo zao. Amefanya balaa kwenye kolabo kama Kiboko Yangu ya MwanaFA, amefunika mbaya katika Nisamehe ya Baraka The Prince na nyingine nyingi. Ana sauti kali ambayo anajua kuipangilia. Anapanda, anashuka.

Ni wasanii wachache sana wenye sifa ya namna hiyo duniani na ndiyo maana Kiba ameendelea kuwa Kiba miaka yote Bongo. Hata anayejiita mpinzani wake, anasifika kwa kutoa nyimbo nyingi ambazo mara nyingi zimegeuka kuwa kama big G lakini Kiba hata sasa akiimba Cindelera, bado mashabiki wataifurahia
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo anayejiita mpinzani wake ndiyo amemfunika katika maeneo yote uliyoyataja.
    1. Collabo ningi za ndani na nje ya nchi
    2. kutoa HIT SINLGES nyingi zaidi
    3. kuwa enterpreneur ( mjasiriamali) kwa kubuni biashara nyingine zaidi ya Muziki
    4. Kuwekeza kwenye majengo ndani na nje ya nchi
    5. Kupiga shows nying na maeneo mengi zaidi eg Dubai, Mombasa, Zambia, UK, Sweden, US etc.

    ReplyDelete
  2. hakuna aliemfunika king sauti yake peke rhythm za kipeke na kila wimbo uko kivyake sio mawibo ya hao ni hayo kwa hayo sauti hizo hizo so nyie mnaoropoka ovyo niwachochezi leave them alone

    ReplyDelete

Top Post Ad