Lisu Aikana Tweet Iliyosambaa Kwenye Mitandao ya Kijamii Kuhusu Ali Kiba na Diamond

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lisu Aikana Tweet Iliyosambaa Kwenye Mitandao ya Kijamii Kuhusu Ali Kiba na Diamond
Mwanasheria wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameikana akaunti ya Twitter iliyoandika maoni kumpongeza mwanamuziki Alikiba, huku ikiwa na picha ya wanamuziki wanaofanya kazi chini ya lebo wa Wasafi.

Lissu amesema hafahamu chochote kuhusu akaunti hiyo na maoni yaliyotolewa akitaka mwandishi amfafanulie.

“Wananisingizia kaka ni wimbo gani wa Alikiba?” akimaanisha haelewi chochote kinachoendelea kuhusu uwepo wa wimbo wa “Seduce Me.”

Amesema akaunti hiyo si yake: “Hiyo akaunti ya Twitter si yangu na nilishasema tangu mwaka jana kaka.”

Jana Agosti 29, akaunti hiyo ilikuwa gumzo kwenye mitandao ikiwa imebeba ujumbe unaosema: “Hakuna kitu kibaya kama wanaume sita kuvaa mawigi kupambana na mtu mmoja. #seduceme#.

Tweet hiyo iliambatanishwa na picha ya Kundi la Wasafi wakiwa wamevaa mawigi ambayo waliitoa sambamba na wimbo wao wa “Zilipendwa”.

Mashabiki wanaomuunga mkono Alikiba walifurahi wakiamini kiongozi huyo amejiunga na wengine wengi ambao walijitokeza hadharani kumpongeza Alikiba.

Baadhi ya viongozi waliompongeza Alikiba ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla; Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KUMBE WANAMPAISHA NA ACCOUNT FAKE ACCOUNT ZA WATU!!!!!!

    ReplyDelete
  2. hapaishwi ni bahati yake usisafiri na nyota ya mwenzio huyu ni king kiba hata kama account hio ni fake tayari ananguruma hadi watu wana haha mara watoe nyimbo utadhania wako kwenye kwaya kaona mhh hapa hatukufaulu nufanye nini bi ajuza ukuje dar tufunge ndoa pia hakuna alie jali sasa haya yote ni wanajipaisha lakini wameanguka 0% na kiba ndio king unalo hilo

    ReplyDelete

Top Post Ad