Lucy Komba Atoa Povu Kwa Wanaomponda Hamisa Mobeto Kuzaa na Diamond...Amtupia Dongo Zari Hassan

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lucy Komba Atoa Povu Kwa Wanaomponda Hamisa Mobeto Kuzaa na Diamond...Amtupia Dongo Zari Hassan
MWANAMAMA aliyewahi kuwika miaka ya nyuma kunako tasnia ya filamu Bongo, Lucy Komba, amejikuta akipoteza sifa ya mwanamke mvumilivu baada ya kutoa povu kwenye ukurasa wake wa Instagram, chanzo kikiwa ni Hamisa Mobeto.

Nyongo ya mwanamama huyo ilitibuka baada ya kuona baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii wakimshambulia kwa maneno Hamisa Mobetto, kuhusiana na mtoto aliyejifungua hivi karibuni, hali iliyompelekea kukumbuka vichambo alivyowahi kuvipokea kuhusiana na ndoa yake.


Samahani lakini kimenichoma, Mabogas ya TZ yanamponda Mtanzania mwenzao, yanamsifia Bogas, sijui yanadhani yatapewa ule urithi, mbona Waganda hawambabaikii? Acheni umaskini wa kujirahisisha. Au mnafikiri mtapitishiwa kila mmoja karanga mojamoja ya bure?”

Na baada ya posti hiyo akaona haitoshi muda mfupi baadaye akaposti tena picha ya Hamisa akiwa na mtoto wake wa kwanza, Fantasy, na kuandika maneno yafuatayo:

“Hongera mwanamke mwenzangu, wanajifanya roho ngumu tu kukuponda wakati roho zinawauma, unatoa vitu hasa mwanamke unazaa huku unatabasamu, wale wanaoniponda ningekuwa mzalendo nisingeolewa na Mzungu;

Ndiyo nimeolewa na Mzungu sababu sina ubaguzi wa rangi wala ukabila na tangu nimeolewa sijawahi kutukana kaka zangu wa Kiafrika, kwa hiyo lazima mjue kutofautisha A na B;
“Pili anayewapa taarifa nimeachwa nahisi kama kachelewa kuwataarifu halafu mwambieni awape taarifa kamili maana huwa anaingia Insta na kuzizungusha bado hajawapa taarifa za kunichamba;

“Ukweli unauma mmepewa ukweli kwa huyo mgeni wenu aliyenenepesha miguu, kiuno kimeshindikana kukipunguza mnalia, chambeni tu mniongezee Followers maana nilikuwa sijaamka bado kujua kumbe umaarufu wa Bongo unatokana na vichambo” ameandika Lucy Komba.

NA ISRI MOHAMED/GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sema Lucy usiogepe wanafki wako wengi, huko wanasifia, huku wanaponda. wanfikiri watapewa Karanga... hahahaaa Hamisa kajua kumtoa nishai bi Mavuzi, anahangaika kupiga picha aonekane mtoto mbichiiii, kumbe grann.

    ReplyDelete
  2. kashushuka! alijiona yeye ndo anakizazi. na kumtukana Wema, Karma imemrudia Mwanaume mwenyewe kitombi haachi mtu ampite, kiko wapi paka poda mpaka ziishe but Mobeto kiboko yako.

    ReplyDelete
  3. he hehe zari umepata kiboko yako for your information wewe unamzaa hamisa grand ma umepitwa na wakati utabaki kupiga picha za kila aina rembukeni wenzako ndio wata babaika hamisamobeto kakuchanganya humpati hata kidole chake cha gumba Mtoto wa kitanzania huyu sio wa mchezo mchezo wee chezea mobeto

    ReplyDelete
  4. we piga picha selfie uimbe garni unajibabaisha tu grandma roho inapwita tumbo joto maskini wee unamjua Naseb au unamsikia that is just a begining subiria picha grandma nilikwambia Humuezi Naseb sasa katayari

    ReplyDelete
  5. Sasa Nyinyi wote hapo ndio kusema. Mnataka kusema mwezenu ni muhenga au. Basi kama ni muheng basi toleo jipya sio la zamani. Hata hamisa mwenyewe muda si mrefu nae atakuwa muhega tu

    ReplyDelete

Top Post Ad