Masau Bwire Aonekana Kukerwa na Kelele za Mashabiki wa Simba na Yanga Asema Aoni cha Kujifunza Katika Mechi Hiyo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Masau Bwire Aonekana Kukerwa na Kelele za Mashabiki wa Simba na Yanga Asema Aoni cha Kujifunza Katika Mechi Hiyo
Msemaji mkuu wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire ameonekana kukerwa na kelele za mashabiki wa Simba na Yanga huku akidai kuwa timu hizo hazina mpira wa kuvutia zinapokutana.

Masau Bwire amesema inapokaribia pambano la watani wa jadi kati ya Simba na Yanga watu wanakosa raha mitaani kwa makelele ya mashabiki wao lakini inapofika siku ya pambano uwanjani hakuna chochote wanachokionesha zaidi ya vurugu na utoto.

“Nikuambieni hawa jamaa hawana lolote hasa kama unazungumzia uwanjani, Mimi naona ni mambo ya kitoto tu, gumzo kubwa kila sehemu mtaani hadi hatuna raha inafika siku yenyewe labda tutapata cha kujifunza lakini unakuta ni vurugu na utoto unatawala uwanjani sioni cha kujifunza kwa kweli”,amesema Masau Bwire kwenye mahojiano yake na waandishi wa habari.
Kauli hiyo ya Masau Bwire imekuja katika kipindi hiki ambacho mashabiki wa Simba na Yanga wanasubiri pambano la mechi ya ngao ya hisani hapo kesho jumatano Tar 23 2017
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unatafuta Kiki wewe mwenyewe huna lolote hebu nyamaze usitake kutuharibia siku

    ReplyDelete

Top Post Ad