MBOWE: Kilimanjaro Hatutegemei CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa mkoa wa Kilimanjaro hawategemei CCM kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo na kusema kitu pekee ambacho kinafanya mkoa huo kuwa wa mfano kwa mageuzi ni kutokana na elimu.


Freeman Mbowe amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Machame Uroki katika ziara yake ya jimbo na kusema kuwa Kilimanjaro inakuwa kimaendeleo kutokana na baadhi ya wazee miaka hiyo kupata elimu ya kutosha ambayo ndiyo imekuwa chachu ya maendeleo hayo.

"Sifa kubwa ya kwanza katika taifa hili kuhusu mkoa wa Kilimanjaro ni elimu, wazee wetu walisoma siyo wote ila wachache waliosoma walisoma sana kulinganisha na mikoa mingine kwa hiyo maendeleo ya Kilimanjaro hayategemei CCM, bala maendeleo ya Kilimanjaro yalikuwepo hata kabla ya uhuru watu walisoma siku nyingi na watu walipata imani siku nyingi, sifa hii ni lazima tuirejeshe, tuna shule nyingi lakini shule nyingi ni zile ambazo hazina sifa ya kuitwa shule" alisema Mbowe 

Aidha Mbowe aliwataka watu kuwekeza nguvu kubwa kwenye elimu kwa watoto wao kutokana na ukweli kwamba ardhi ya kuweza kuwarishisha watoto kwa sasa haipo Kilimanjaro hivyo wanapaswa kuwekeza zaidi na zaidi kwenye elimu na kusema anatambua kuwa wanafanya hivyo ila bado haitoshi wanapaswa kuongeza nguvu zaidi na zaidi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huu si ubinafsi bali ukweli. Watu tuache majungu, tuache siasa. Ukweli ni kwamba, Elimu ni ufunguo wa maisha. Ykupata elimu bora, ukajitambua na kujituma utapata maendeleo. Mikoa mingi elimu tabu. Kuna kelele nyingi za kutaka kujipatia pesa, lakini adabu inayotakiwa ili upate maendeleo ni shida. Pia ukiwa na elimu, ustaarabu pia upo. Wengi wetu yunafikiri pesa ni maendeleo si kweli. Maendeleo yanaendana na elimu bora na ustaarabu wa namna ya pekee. Si wote wenye pesa ni wastaarabu.Kuna adabu hawana na hawajijui.Bila ya adabu ya pekee itokanayo na elimu inakuwa ni vigumu sana hata katika undugu, Hurudisha jamii nyuma kabisa.Elimu inamwezesha mtu kufikiri, kujituma, kujitegemea, kuwa maridadi.Ni elimu ndio inahitajika ili tujikomboe kifikra. Wengi wasiosoma inakuwa shida kutumia akili zao vipasavyo.

    ReplyDelete

Top Post Ad