Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jaguar ameandika maneno akisema kuwa bila wao asingefanikisha hilo, huku akiwashukuru wapinzani wake kwa kukubali ushindi wake huo.
"Hakuna linalowezekana bila Mungu, Nawashukuru watu wa Starehe kwa ujasiiri na kuniamini kuwawakilisha bungeni, nawashukuru wote walioniunga mkono , marafiki, familia ambao walikuwa nami wakati wa kampeni.
Na Pia nampongeza mpinzani wangu Steve Mbogo, Boniface Mwangi na Mh. Kwenya ambao waliweka kampeni safi. Huu sio ushindi wa Starehe tu bali ni ushindi wa vijana wote nchini Kenya ambao wameona mbele, sasa tuijenge Starehe ile tunayoitaka, Mungu awabariki", aliandika Jaguar.
Jaguar ameibuka mshindi wa Jimbo hilo kwa asilimia 53% ya kura zote, huku akifuatiwa na Steve Ndwiga aliyepata asilimia 31% na Boniface Mwangi akipata aliyepata asilimia 13%.
Wimbi la wasanii Afrika Mashariki kuingia kwenye siasa na kufanikiwa kushinda viti vya Ubunge linazidi kuongezeka, Jaguar atakuwa msanii wa kwanza nchini Kenya kupenya katika siasa na kufanikiwa kuwa Mbunge, wakati nchini Tanzania Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi pamoja na Mbunge wa Mikumi Joseph Haule walifanikiwa kupenya kwenye uchaguzi Mkuu 2015 na kuwa wabunge huku nchini Uganda msanii Bobi Wine naye amefanikiwa kupenya na kuwa Mbunge katika uchaguzi wa marudio uliofanyika mwaka huu.
Jaguar sio wa kwanza. Yupo Mtoto wa Sonko
ReplyDelete