MWIGULU NCHEMBA: Atakaokiuka Sheria za Nchi na Kujiingiza Kwenye Ujambazi na Ujangiri Atafutiwa Uraia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MWIGULU NCHEMBA: Atakaokiuka Sheria za Nchi na Kujiingiza Kwenye Ujambazi na Ujangiri Atafutiwa Uraia
Serikali kupitia wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kuwa inaweza kuwafutia uraia watanzania wapya waliopewa uraia wale ambao walikuwa wakimbizi wanaoishi makazi ya katumba Mishamo na Ulyankulu iwapo wataonekana kushindwa kufuata sheria za nchi na kujihusisha na vitendo vya uharifu na uvunjifu wa sheria za nchi,vitendo vya ubaguzi wenyewe kwa wenyewe ubaguzi wa kitabaka kubaguana kisiasa, kidini na kwa namna yeyote hawawezi kuvumiliwa hata kidogo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba wakati akiwahutubia raia hao wapya kwenye Makazi ya Katumba Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wakati akiwataka kujiepusha na vitendo vya kubaguzi.

“Mimi najua uraia usiofutwa ni ule wa kuzaliwa mtu kama akishazaliwa kama ni Muafrika ata akiandikishwa kwingine anaendelea kuwa Muafrika. Lakini kama watu wanafanya vitu vya kinyama ambavyo hatujazoea na ubaguzi huo ndio uliosababisha matatizo kule hatuwezi tukaamisha matatizo kutoka kule tukayaishi tukiwa huku kama ugomvi kule ulizuka na watu wakakimbia yaliyogombana hayakuwa mabonde nama milima yalikuwa ni hao hao watu,” alisema Mwigulu.

“Kwahiyo ukianzisha ubonde na ummlima ukauhamishia hapa unaleta ugomvi ambao sisi hatuuzoea kwa maana hiyo leo naongea kindugu kwa maana hiyo muonyane wenyewe kwa wenyewe ambiazaneni na mkimuona mtu yupo wa aina hiyo kwani nyinyi hamna wazee wambie hilo lina gaharama hapa sio mahali pakee na kwa bahati nzuri kamati ya ulinzi na usalama ipo hapa mtakapo muona mtu anafanya kaubaguzi wataweka mapendekezo na hamtajua ni saa ngapi wameweka kwahiyo kama mnapendana shaurianeni mapema sana hatutaki kusikia lugha za huyu anakaa juu anakaa bondeni hayatusaidii sisi hapa kwa yoyote atakae thibitika ni jangili,jambazi nitafuta uraia wake hatutampa muda wa kuchomoa chaji kwenye soketi tuamuondoa.”

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad