Tundu Lisu Apingwa Mgomo wa Mawakili Nchi Nzima

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tundu Lisu Apingwa Mgomo wa Mawakili Nchi Nzima
Wakili wa kujitegemea na mmiliki mwenza wa Smile Stars Attorneys, Leonard Tungaraza Manyama amepinga wito uliotolewa na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kutaka wanachama wote wa TLS kususia kwenda mahakamani kwa siku mbili.

Akiongea na waandishi wa habari Leonard Tungaraza Manyama amepinga wito huo na kuwataka Wanachama wote wa TLS kuendelea na shughuli zao kama kawaida na amewataka watendaji wa TLS kutoigeuza taasisi hiyo kama chama cha siasa au taasisi inayoendesha shughuli zake kwa mtindo wa kiharakati na badala yake kibaki kwenye majukumu yake ya kutoa huduma kama taasisi ya kitaaluma.

Aidha Manyama amesema yeye kama mwanasheria na mwanachama wa TLS, amesikitishwa na tukio la shambulizi kwenye ofisi za IMMMA Advocates na kuitaka TLS kutoa muda kwa vyombo vya dola kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Mbali na hilo Manyama amedai mawakili na wanasheria ni watumishi wa idara ya mahakama na kwamba tukio lolote la kutofanya kazi katika siku mbili hizo kutaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi wa kipato cha chini ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta haki zao kwa muda mrefu, huku mpango wa kuhakikisha kesi za muda mrefu zinapunguzwa mahakamani nao ukikwama.

Leonard Tungaraza Manyama ameibuka siku moja baada ya Rais wa TLS  Tundu Lissu kuwataka mawakili kutohudhuria kwa siku mbili shughuli za mahakama Jumatatu na Jumanne kama ishara ya kulaani tukio la shambulizi lililofanywa kwenye ofisi za kampuni ya mawakili ya IMMMA    
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tao Uoga We Mwanasheria. Uwaonee huruma wenzako wanaohatarisha maisha yao kupitia Kazi zao. Huwezi jitenga na kundi kuzalisha kundi la kisiasa. Afadhali ungekaa kimya na kwenda ofisini kwako kwa kupinga. Huu si uzalendo, sheria ndo wanazitetea na kuzilinda, usipokuwa huru kufanya kazi yako ndo sawa na wafanyao kazi kwa woga. Bi Karume mwanamke shujaa unachogombea hapa ni nini. Kujipendekeza au kutokujua uzito wa jambo hili, wote tumesoma lakini si wote wazalendo. Si wote wanahekima na akili sawa. Nguvu itawale na si udhaifu uliouonyesha, je kesho kwako nani atakuunga mkono na kukutetea. Serikali yetu imeacha kufuata katiba mya na sheria safi kuepusha haya, we kama mwanasheria unapuuza ninawasiwasi na elimu yako kama si yakubabaishia basi si mtu wa kukuamini hata. Ungepigania haki kwa kuungana na wenzako. Umoja ni nguvu utenhano ni udhaifu. Ombea Mungu yasikupate ndipo utakapokosa jumuia.

    ReplyDelete
  2. Tungaraza...!!! Wewe ni Dume tena Dume la Shoka.. Msimamo wako ni wa Haki na Ukweli na wenye Dhamira kusudiwa kwa Wadai Haki.

    Lizu ni Mpotoshaji na Ni Mchozhezi na anaeleweka Hivyo. Hata Tasfsiri Nyingine.
    Lizu Ni mpenda Popularity ambayo Hastahiki.
    Lizu Ni mtu wa kujibamiza anapo hisi au kuona atapata masilahi binafsi.
    lizu ni Mlala hoi wa zamani ambae kapewa Ulaji kiulaini kwa Kuuza Maneno(Soko limemdororea NOW)
    Lizu ni mtafuta mbinu na Njia mbadala kutaka kubadilisha Uenyekiti wa chama alichokaribishwa.
    Lizu ni Mlafi mwenye kujali masilahi yake binafsi na yuko tiyari kumsemea na kumpigia dede
    atakae mlipa na kwa muda fulani ( sawa sawa na banda la simu za barabarani kwa dakika)
    Lizu ni mmoja ya wenye ndoto za mchana kwamba anaweza kuanzisha chama akihama hapo alipo.
    Kizu ni kijana aliekuwa na Tamaa na Utashi wa kuto tosheka na alicho nacho including Elimu
    Kizu ni kwa sasa hana msimamo na hajui Malengo yake Tarajiwa atumie mbinu zipi ili afikie huko.
    Kizu ni Mpotoshaji na Mchanganya Mada ambe amepoteza Mwelekeo. (Yupo Yupo Tu)

    Kwa Ujumla huyu kijana anahitaji Mapumziko/Apumzishe kunako stahili mapaka turidhike/Aridhike
    kwamba afya yake Kiakili na Mwili inaanza Kuimarika na Kurudia Hali Halisi ya Mwanadamu inavyo takiwa.

    Tungaraza wewe ni Mzalendo na Umweza Kuona Ubatili wa Fikira za Huyo Mchochezi ambae atakuwa na Shtaka la kujibu siku za Usoni. Proffesionally he is second to minus One equivalent to Fedeliki Smaye( As they share in the common, (Round figure).

    Tungaraza Endelea na Uanasheria wenye Tija na Uwaache hao " Mabahaluli" Wanaojaribu kubahatisha bahati zao kama wanadhani kuna Mabahalluli ambao wanaweza Kuwa sikiliza na kuwafata.
    Amepiga Hola. Tanzania Ni ya Sasa ni ya Kidigitali na si ya Analogi ambayo wao bado hawajaelewa na kufahamu kwamba
    Mwamko ni mpya...!!!
    Dhamira ni Mpya..!!!
    Nia Njema ya Utawala ni Mpya...!!!
    Raisi Wetu na Serikali Ni Mpya...!!!
    Kwa Nia ya Kuijenga TANZANIA MPYA....!!!!

    Kalaga Baho LIZU.....

    ReplyDelete

Top Post Ad