Vita Kuu ya Mtoto wa Mobetto Yeendelea Huku ikimwacha Zari na Kilio Mobetto Kicheko

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Vita Kuu ya Mtoto wa Mobetto Yeendelea Huku ikimwacha Zari na Kilio Mobetto Kicheko
HALI si shwari kati ya mwanamitindo matata wa Bongo, hamisa hassan Mobeto na mwanamama mjasiriamali wa Afrika Mashariki ambaye ni mzazi mwenza wa msanii wa Bongo Fleva, Zarinah hassan ‘Zari The Boss Lady’, kisa kikielezwa kuwa ni mtoto.

Wakati mtoto huyo wa Mobeto aliyepewa jina la baba mzazi wa msanii huyo akitimiza siku 14 leo Jumatatu, uzao huo umesababisha Mobeto kuibuka na kicheko kwa kuungwa mkono na Wabongo huku Zari akidaiwa kuambulia kilio kutokana na kushambuliwa mitandaoni.

Mara tu baada ya Mobeto kujifungua mtoto huyo Agosti 8, mwaka huu, Zari alitokwa na povu ambalo siyo la nchi hii huku akipiga mkwara kuwa asihusishwe na mtoto huyo wa ‘bitch’ (malaya), kauli ambayo aliitoa kupitia ukurasa wake unaotambuliwa kwenye Mtandao wa Instagram. Kilichofuatia ni majibizano ya mashabiki wa Mobeto na wale wa Zari ambapo kila upande ulikuwa ukivutia upande wake, lakini pande zote zilichukizwa na neno ‘bitch’ ambalo ni tusi lililotumiwa na Zari kwenda kwa Mobeto ikielezwa kuwa lilitokana na hasira.

JINA LA BABA MkWE
Wakati mambo yakiwa hayajakaa sawa huku mtoto huyo wa pili wa Mobeto akiibua tafrani ya aina yake mitandaoni, mwanamitindo huyo aliibua lingine baada ya kumpa mtoto huyo jina lililodaiwa kuwa ni la baba mkwe wa Zari. Inasemekana kwamba, jambo hilo ndilo linalodaiwa kuthibitisha kuwa Mobeto amezaa na mwanaume huyo hivyo kuibua shangwe kwa Wabongo na kumuongezea machozi Zari.

Ilielezwa kuwa, jina hilo, ndilo lililomaliza maswali mengi ya mashabiki ambao walitaka kumjua baba wa mtoto huyo. Awali, Mobeto alifungua akaunti kwenye Mtandao wa Instagram kwa jina ‘Tanzania Baby’, lakini baadaye wiki iliyopita alibadilisha jina hilo ambapo hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, akaunti hiyo ilikuwa ikikaribia kuwa na wafuasi (followers) laki moja.

MAMA MZAZI NA DADA MTU
Tukio lingine lililoibua gumzo juu ya mtoto huyo ni kufuatia kitendo cha mama mzazi wa jamaa huyo na dada yake kuonekana kwa nyakati tofauti wakiwa kwenye hospitali ambayo Mobeto alijifungulia, ikidaiwa kuwa walifuata damu yao ambayo ni nzito kuliko maji.

Hata hivyo, jambo lingine lililozungumzwa zaidi ni kitendo cha jamaa huyo kumkana Mobeto ikidaiwa kuwa alilenga kumpooza Zari ambaye inasemekana jambo hilo lilimtibua mno na kumtaka jamaa huyo aliyezaa naye watoto wawili kukanusha kuzaa na Mobeto.
mobeto na zari
Mobeto.


MOBETO APIGWA STOP
Katika mazingira hayo, mtu wa ndani ya familia ya mwanaume huyo alilitonya Ijumaa Wikienda kuwa, kwa sasa Mobeto amepigwa ‘stop’ (marufuku) kufanya mahojiano na waandishi wa habari.

Hata hivyo, Ijumaa Wikienda lilifika nyumbani kwa Mobeto, maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar ambapo mara baada ya kujitambulisha lilifungiwa mlango wa geti kwa madai kwamba, waandishi hawahitajiki.

WAZAZI FULL RAHA
Kwa upande wao, wazazi wa mwanaume huyo anayedaiwa kuzaa na Mobeto, wamepokea baraka hiyo kwa mikono miwili huku babu mtu akifurahia zaidi mtoto huyo kupewa jina lake. 40 YA kiShiNDO Hata hivyo, taarifa zilizolifikia gazeti hili muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni zilieleza kwamba, familia ya Mobeto yaani mama yake ipo kwenye mipango kabambe ya kuandaa 40 ya mtoto huyo kwani itakuwa haijawahi kutokea Bongo. Tusubiri!


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jamani kwa nini alie mbn waislamu tumeruhusiwa wake wanne halafu isitoshe is she zari entitled na diamond au kwani kaolewa Hamisa mtoto mbichi bado anadai bwana wakati yeye huyo bi kizee kanyakua diamond si alikuwa na mchuchu wake mwenzake alilia mwisho akamuachia na sasa lia weee halafu utanyamza kwanza huna haya diomond unamzaa kabisa sura yako mikono na shingo inaongea bwana umri utadanganya lakini kiwili wili chako kinaongea dada uko kwenye 48 50 so tulia ulee watt sio kuhangaika na dunia kujizuzua rudi kwa mola wako ogopa kesho akhera kuna moto huko tubia sali kabla hujasaliwa kaulize mashehe wakufafanulie hayo unayo yafanya bibi we dunia tunapita njia kazi huko kwenye ???? utajibu nini

    ReplyDelete
  2. kwana bi kizee ni mwuislam? si alifata dini ya Ivan, anafikiri kumzalia Dai ndo hatopenda tena, kashachanganyikiwa huyo hana jinsi.

    ReplyDelete
  3. Domo kashtuka kaona watoto wa Zari ni wengi kulea, bora na yeye aongeze kwa mtz mwenzie. pole Ajuza paka poda nyingi uonekane kijana bitch.

    ReplyDelete
  4. zari kwa wa TZ umefika umepitwa na wakati dada utaita bitch utapaka makeup umalize kujipodoa na mawigi ya kila aina ujizuzue lakini mobeto kiboko yako hebu kuwa na haya una watt wakubwa huyu mkubwa si rika mmoja na diamond jamani

    ReplyDelete
  5. hee makubwa ya bi mkubwa una ngangania kuolewa tena unataka harusi iwe siku ya kuzaliwa ya queen hamisa mobeto hio si ndio raha jamani hivi kama daimondi alikuwa anaishi tandale kweli bi ajuza ungw ngangania hivo wee huko kwenu hakuna wanaume hata hivo unahangaika bure hamisa ni yule yule wala habaishwi na pisha pisha zako makubwa haya yakutaka kuolewa kwa nguvu hebu kabadili dini kwanza hujijui huji tambui maskini wee

    ReplyDelete
  6. Wabongo bwanaaa.....utandani ndo mlishika miguu wakati wanatiana mimba. Huyo Mobeto ana midume mingapi hapa mjini mpaka mkomae na Diamond. Mwanaume rijali akikataa mtoto ujue hapo kuna utata mashoga muelewe mafara nyie. Mwambieni huyo bitch Mobeto akapime DNA asitake kutafuta kiki kupitia migongo ya watu hapa pumbavu.........Alikaa na mimba hakusema mwenye mimba ni nani mpaka kazaa ndo anajifanya kutaka kupaka watu matope kwa nini???!Mlikua wapi kumzalia diamond mpaka mmeona Zari kutuliza akili ya D na sasa anafocus kazi zake mnaleta madanga yenu nyoko nyieeeeee....kafieni mbali huko hakuna wa kubambikiwa mtoto na malaya bongo hapa........

    ReplyDelete

Top Post Ad