Wenyeviti 50 wa Serikali za Mtaa wa CUF Wamuunga Mkono Profesa Lipumba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wenyeviti 50 wa Serikali za Mitaa  wa CUF Mkoa wa Dar es Salaam wametangaza kuunga mkono uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF la upande wa Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa vua uanachama wabunge  wanne wa viti maalumu na madiwani wawili.

Wabunge waliovuliwa uanachama ni  Halima Ali Mohamed, Khadija Salum Ally,  Salma Mohamed Mwasa, Miza Bakari Haji, Raisa Abdallah Mussa, Riziki Shahari Mngwali, Saumu Heri Sakala na Severina Mwijage.

Wakiwakilisha wenzao 36 wenyeviti 14 kutoka mitaa mbalimbali ya halmashauri za manispaa tano  za Dar es Salaam wamesema wamefikia hatua hiyo baada ya kuridhisha na kazi nzuri inayofanywa na Profesa Lipumba.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake 14 mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Keko Mwanga B, Shilingi Shilingi amewaambia wanahabari  leo Jumanne Agosti 8 wanaunga mkono uamuzi wote wa Baraza Kuu la Uongozi kwa kuwa wabunge hao wamebainika kukihujumu chama hicho.

"Tunamtambua Maalim Seif Sharif Hamad kama katibu mkuu lakini kwa sasa nafasi yake inakaimiwa na Magadalena Sakaya kutoka na yeye kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya CUF," amesema Shilingi

Mbali na hilo Shilingi amewataka watu wanaoingilia mgogoro wa chama hicho kuacha mara moja na kwamba mgogoro ni wa kikatiba na suala hilo lipo mahakamani muda si uamuzi utatolewa.

Mwananchi:
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Siasa Chafu, zinapoungwa na Wananchi na wakitumika na wanasiasa, si ushindi, si maendeleo, na si ufanisi. Nchi yetu imeepushwa na mengi lakini kwa ujinga unaofanyika na viongozi wetu wengi walio madarakani. Nchi hii inajigawa vipande vipande kila siku. Na hii ni mbaya. Maendeleo ya wote hayataletwa kwa njia hizi. Mtakaposhtuka, haitaponyeka tena.Ni Watanzania wenyewe mnaligawa taifa kwa uchu wa kutaka madaraka.Mko radhi damu imwagike kwa kuwa viongozi.

    ReplyDelete

Top Post Ad