Wolper Alizwa na Umati wa Vijana Uliojitokeza Jana Kufanya Usail TRA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wolper Alizwa na Umati wa Vijana Uliojitokeza Jana Kufanya Usail TRA
Msanii wa filamu bongo, Jacqueline Wolper aumizwa baada ya kuona idadi kubwa ya watu waliojitokeza kufanya usaili wa TRA jana na kusema anawaonea huruma yatima ambao hawana mtu wa kuwapigania ili kuweze kupata kazi hizo.

Wolper amebainisha hayo baada ya picha iliyokuwa ikionyesha umati wa vijana waliojitokeza kwa wingi kufanya usaili  wa TRA kwa awamu ya kwanza ambao umefanyika jana na kuendelea leo ambao umeandaliwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

"Nikiangalia picha kama hizi naumiaga sana na nilivyo na machozi ya karibu basi nalia kabisa. Yaani naona hata wadogo zangu ni miongoni mwa hawa wanaopigania nafasi ya kupewa kazi na ukizingatia nimesomesha kwa tabu sana tena nilikuwa sina hata biashara huku nikisaidiana na wazazi wangu. Roho inauma pale ambapo mdogo wako anakwambia Dada nimepata kazi ya kujishikiza kwa wiki tatu nitalipwa laki na nusu kule Mkoani Mbeya kijijini tena hapo ni uliyemfikiria akipata 'degree' yake atakuja japo kuinua familia ama ajitegemee mwenyewe lakini siyo hivyo", aliandika Wolper.

Pamoja na hayo, Wolper aliendelea kwa kusema "mimi najiuliza unaposema ipo siku sijui hiyo siku ni ipi. Haya wote hao waliojitokeza huku wanaohitajika ni wachache yaani kwa uwiano ni kama mtu mmoja achaguliwe kati ya watu 140 kwa sababu ni watu 56,000 kwa nafasi 400 kama 'data' ziko sahihi, Mungu wangu bora hata mdogo wangu ataomba hela ya vocha na kula na kulala atapata. Lakini vipi waliyosomeshwa na wazazi wa kambo au kwa msaada", alihoji Wolper.
Huu ndiyo ujumbe aliyoandika Wolper katika instagram yake.

Jacqueline Wolper siyo mtu wa kwanza kuonyesha hisia zake juu ya tukio lililotokea siku ya jana katika usaili huo kwa maana kila aliyeweza kuona picha hiyo hakuweza kujizuia kutoa dukuduku lake la moyoni.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad