Yanga Kumchezesha Kipa wa Serengeti Boys Leo kwa Majaribio

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Yanga Kumchezesha Kipa wa Serengeti Boys Leo kwa Majaribio
Kuna uwezekano mkubwa kwa kipa chipukizi wa Yanga, Ramadhan Kabwili, leo Jumamosi kwa mara ya kwanza akakaa langoni kuichezea timu yake hiyo dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.

Uwezekano wa Kabwili aliyejiunga na Yanga hivi karibuni akiwa kipa namba moja wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys, kucheza mechi hiyo umekuja kutokana na wenzake kuwa majeruhi.

Makipa Rostand Youthe na Beno Kakolanya wanaopokezana langoni, wote hawakufanya mazoezi ya Yanga juzi na jana Ijumaa kutokana na kuwa majeruhi, hivyo Kabwili ana nafasi kubwa ya kucheza leo. Daktari wa Yanga, Edward Bavu, ameliambia Championi Jumamosi kuwa:

“Makipa wetu wawili Rostand na Kakolanya bado ni wagonjwa lakini wanaendelea vizuri, hivyo katika mechi ya kesho (leo) tunaweza kumtumia Kabwili. “Matarajio yetu ni kwamba Rostand atakuwa fiti hivi karibuni na ataungana na wenzake haraka iwezekanavyo baada ya kuumia mgongo, wakati Kakolanya yeye akiendelea na matibabu ya goti.”

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad