Yanga Yampa Tshishimbi Gari la Milioni 100

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Yanga Yampa Tshishimbi Gari la Milioni 100
BAADA ya kelele za kumsifu kuwa nyingi, Yanga imempa kiungo wake Papy Kabamba Tshishimbi gari la kutumia lenye thamani ya Sh milioni 100. Tshishimbi anasifiwa kwa kufanya vizuri katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Jumatano wiki hii.

Fasta baada ya mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga ikafungwa kwa penalti 5-4, kiungo huyo alikabidhiwa gari likiwa na dereva wake kwa matumizi binafsi. Yanga imeamua kumpa Tshishimbi raia wa DR Congo gari hilo aina ya Ford Ranger lililo katika muundo wa ‘Double Cabin’ lenye rangi ya chungwa na jana alionekana nalo mazoezini Uwanja wa Uhuru.


Papy Kabamba Tshishimbi akiingia katika gari alilopewa aina ya Ford Ranger lililo katika muundo wa ‘Double Cabin’ .

Gari analotumia Tshishimbi kama ukilitaka jipya lake utalazimika kutoa si chini ya Sh milioni 100, kwa kuwa ndiyo bei yake kwani mengi yake ni mapya na yanatoka kiwandani Afrika Kusini. Tshishimbi amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Klabu ya Mbabane Swallows ya Swaziland na baada ya kucheza mechi mbili tu, amejizolea umaarufu mkubwa nchini.

Championi Jumamosi jana asubuhi lilimshuhudia Tshishimbi akiwasili katika mazoezi ya Yanga akiwa ndani ya gari hilo akiendeshwa na dereva maalum na baada ya mazoezi hayo aliondoka naye. Bosi mmoja wa Yanga akigoma kutajwa jina lake, alisema: “Tumempa gari Tshishimbi kwa matumizi yake ya kawaida kama kwenda mazoezini na kurudi, hili ni jambo la kawaida kwetu.

“Huyu kiungo anakaa Mbezi sasa bila gari anaweza kupata tabu ya kuwahi mazoezini ukizingatia ni mgeni hapa nchini, gari hili atalitumia katika muda huu na yeye analitumia tu.” Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, alisema: “Hilo gari Tshishimbi analitumia tu kwa kuwahi na kutoka mazoezini kwenda kwake, haimaanishi kama klabu imempa moja kwa moja.”Ten alisisitiza kuwa, Tshishimbi atalitumia gari hilo kwa matumizi ya kawaida na isieleweke kwamba amepewa ‘mazima’. Mbali na Tshishimbi ambaye analitumia gari hilo, Amissi Tambwe yeye ana gari binafsi Toyota Land Cruiser pia Ibrahim Ajibu anamiliki gari aina ya Toyota Brevis alilolipata baada ya kusajiliwa na Yanga akitokea Simba.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yan nyie wazembe kweli ata picha ya gar kugoogle mmeshindwa?

    ReplyDelete

Top Post Ad