Kubenea aelezea yaliyomsibu Kuugua Ghafla na Kushindwa Kufika Kamati ya Maadili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Ubungo (Chadema) Saed Kubenea amesema aliugua ghafla  akiwa njiani kuelekea katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Amesema aliitikia wito wa Spika Job Ndugai ambaye Jumanne wiki hii alimpeleka mbele ya kamati hiyo.

Spika alisema Kubenea anamtuhumu kwenye mitandao ya kijamii kuwa amesema uongo kuhusu idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.

Kubenea amesema alitakiwa kuripoti mbele ya kamati saa 7:30 mchana lakini alipokwenda aliambiwa kuna shughuli za Bunge zimeingiliana hivyo arejee saa 9:30.

Mbunge huyo amesema hakuweza kurejea mbele ya kamati baada ya kuugua ghafla.

“Nilishaenda kwa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, wakati ninakwenda kwa Kamati ya Maadili nikapata

tatizo,” amesema Kubenea.

Awali, Katibu wa Wabunge wa Chadema, David Silinde alisema Kubenea alikwenda kwenye zahanati ya Bunge baada ya kujihisi vibaya.

“Alijisikia kukosa nguvu akaenda zahanati, amepumzishwa na sasa anasema ni simu yake ya kwanza kuongea nayo tangu

apumzishwe. Ndiyo amekaribia kumaliza dripu,” alisema Silinde.

Daktari wa zahanati ya Bunge, Noel Solomoni alithibitisha kupumzishwa kwa mbunge huyo tangu saa kumi jioni.

Mwananchi:
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad