Lwandamina, Cannavaro Waamua Kumfuata Manji Mahakamani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lwandamina, Cannavaro Waamua Kumfuata Manji Mahakamani
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amekwenda moja kwa moja hadi katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kuteta na bosi wake wa zamani, Yusuf Manji.

Lwandamina alikutana na Manji katika viwanja vya mahakama ya Kisutu akiwa ameongozana na wasaidizi wake kam Shadrack Nsajigwa akiwemo Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali 'Mensah' na Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh.

Naye nahodha wa Klabu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, leo  ameibuka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar na kupata nafasi ya kuzungumza na aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Yusuf Manji.

Baada ya kutinga mahakamani hapo, Cannavaro alimuwahi Manji na kusalimiana naye kisha kupiga kuzungumza mambo machache ambayo hata hivyo haijajulikana kama walikuwa wakijadili mambo ya soka kuhusu klabu hiyo au la!

Manji alikuwa mahakamani hapo kutokana na Kesi inayomkabiri Manji kuhusiana na kutumia madawa ya kulevya imeshindwa kusikilizwa leo katika mahakama ya Kisutu na kusogezwa mbele hadi Septemba 25.

Suala la kushindwa kusikilizwa ,limetokana na Manji kuchelewa kufika mahakamani, lakini naye alimueleza hakimu kuwa aliambiwa hakimu yuko katika kikao.

Kutokana na hali hiyo, imesogezwa mbele hadi Septemba 25, Manji atakapotakiwa kuleta mashahidi wake.

Manji anatuhumiwa kutumia madawa ya kulevya, jambo ambalo amekuwa akilikanusha.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad