Polisi Mkoani Arusha Yatoa Taarifa Kuhusu Miili ya Watoto Waliookotwa Jana Kwenye Shimo la Choo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polisi Mkoani Arusha Yatoa Taarifa Kuhusu Miili ya Watoto Waliookotwa Jana Kwenye Shimo la Choo
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limethibitisha kuwa miili miwili ya watoto iliyokutwa jana kwenye shimo ikiwa imeharibika katika Kata ya Olasiti ni miongoni mwa watoto waliotekwa tangu August 21, 2017.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amesema kuwa mtu aliyehusika na utekaji wa watoto anayeshikiliwa na Jeshi hilo baada ya kukamatwa mkoani Geita alieleza jana mchana baada ya uchunguzi akikiri kuhusika kuwateka watoto hao na kuwauwa kisha kuwatumbukiza katika shimo la maji machafu.

Miili ya watoto hao imetambulika kuwa ni Iqram Salum na Maurine David Ernest.

”Alihusika kuwateka hawa watoto na alishawadhuru. Tuliongozana naye mpaka Olasite na kuonesha sehemu ambayo alikuwa amewaua hawa watoto na kuwatumbukiza kwenye shimo la maji machafu katika nyumba iliyojengwa hivi karibuni.”

Aidha, Kamanda Mkumbo amesema wanaendelea kumshikilia mtuhumiwa huyo na upelelezi utakapokamilika atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

“Tunaendelea na uchunguzi na tukimalisha tutamfikisha Mahakamani.” – Kamanda Mkumbo.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad